Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa SDGs nchini Tanzania

Kijana kutoka Tanzania na bango la lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia.
Warren Bright/UNFPA Tanzania
Kijana kutoka Tanzania na bango la lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linalotaka usawa wa kijinsia.

Utekelezaji wa SDGs nchini Tanzania

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s unajadiliwa kwenye jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu au HLPF hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.  Mkutano huu wa kila mwaka umewaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia na pia vijana ambao mchango wao umeelezwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni muhimu katika kutimiza malengo hayo.

Miongoni mwa vijana wanaohudhuria jukwaa hili ni Faustine Benedict Kikove kutoa asasi ya Umoja wa Mataida UNA nchini Tanzania Amenieleza kwamba bila kushirikisha vijana ipasavyo itakuwa changamoto kubwa kwa Tanzania kutimiza malengo haya

(Sauti ya Faustine Kikove )

Mwaka huu tathimini imejikita katika malengo sita ambayo ni, lengo namba 4 la kuhakikisha elimu jumuishi na bora kwa wote, lengo namba 8 la kuchagiza ukuaji endelevu, jumuishi wa uchumi na ajira zenye hadhi kwa wote, lengo namba 10 lililojikita katika kupungusa pengo la usawa ndani na miongoni mwa nchi, lengo namba 13 la kuchukua hatua haraka kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake, lengo namba 16 la kuchagiza jamii zenye amani na jumuishi kwa ajili ya maendeleo endelevu , kutoa fursa kwa masuala ya haki kwa wote, uwajibikaji na taasisi imara na jumuishi katika ngazi zote, na lengo namba 17 ambalo ni la kuimarisha utekelezaji na kufufua ushirika wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo endelevu. Nchi zimepiga hatua gani na mkazo uwekwe wapi kuyafanikisha malengo haya ifikapo 2030. Nikizungumza na John Kalage mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya Haki Elimu nchini humo amesema mafanikio yapo lakini pia changamoto

 (Sauti ya John Kalage)