Watoto 3 wauawa Afrin Syria katika shambulio karibu na shule-UNICEF

12 Julai 2019

Watoto watatu wameuawa katika shambulio dhidi ya shule huko Afrin Kaskazini mwa Syria na kusababisha uharibifu mkubwa wa shule husika limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Katika taarifa ya mkurugenzi wa kanda ya afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati wa UNICEF Geert Cappelaere, UNICEF imeshutushwa na kushangazwa na mauaji ya watoto hao yaliyotokea katika shambulio lililofanyika jana dhidi ya shule. Amesema “shambulio hili limekuja wakati ambapo machafuko yameshika kasi katika sehemu mbalimbali za Syria nchi ambayo imeghubikwa na vita.Katika sikukadhaa zilizopita kumekuwa kukija taarifa za kuuawa kwa Watoto Zaidi katika mapigano kwenye jimbo la Idlib Kaskazini Magharibi ambako Watoto watatu wamearifiwa kuawa na mabomu ya kutegwa ardhini yaliyolipuka kwenye viunga vya mji wa Damascus.”

Cappelaere amesema tangu mwanzoni mwa mwaka huu zaidi ya watoto 140 wameuawa na idadi inaendelea kuongezeka kwa kasi “Watoto wanauawa nchini Suyria kila siku na vita hivi kwa watoto Syria viko mbali sana kumaliza.”

Shambulio la jana amesema lilikuwa kilometa chini ya 100 kutoka katika shule inayosaidiwa na UNICEF na limesababisha uharibifu mkubwa. Kwa bahati nzuri hakukuwana vifo katika shule hiyo ya UNICEF lakini kumeripotiwa hali ya taharuki miongoni mwa Watoto na mshtuko mkubwa kutokana na sauti kubwa ya mlipuko waliyoisikia wakiwa darasani ambayo ilisababisha vioo vya madisha na milango ya shule kuvunjika .

Kote nchini Syria shule 1 kati ya 4 haziwezi kutumika tena kutokana na vita. Mwaka jana mashambulizi dhidi ya shule na vituo vya elimu yaliyoorodheshwa yalikuwa ni idadi kubwa zaidi tangu kuanza kwa vita mwaka 2011.“Watoto sio walengwa, shule ,vituo vya elimu  na wafanyakazi wa shule sio walengwa , kuwa Watoto ni ukiukaji mkubwa wa haki za Watoto na wanaouwa Watoto lazima watawajibishwa” limesema shirika la UNICEF.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud