Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua kubwa yaendelea kuighubika Cox’s Bazar na kusababisha zahma-WFP

Mvua kubwa na upepo vimepiga kambi za wakimbizi Cox's Bazaar nchini Bangladesh tangu Julai 4, 2019.
WFP/Gemma Snowdon
Mvua kubwa na upepo vimepiga kambi za wakimbizi Cox's Bazaar nchini Bangladesh tangu Julai 4, 2019.

Mvua kubwa yaendelea kuighubika Cox’s Bazar na kusababisha zahma-WFP

Wahamiaji na Wakimbizi

Mvua kubwa za Monsoon zinazoambatana na upepo mkali zimeendelea kughubika makambi ya wakimbizi wa Rohingya katika enepo la Cox’s Bazar nchini Bangladesh tangu Julai 4 na kusababisha hasara kubwa ikiwemo Maisha ya watu, kutawanya watu wengine 5,600 na kuathiri maelfu ya nyumba.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wakimbizi walio katika hali mbaya zaidi wameahamishiwa kwenye maeneo salamaambayo ni makazi mapya kambini hapo.”Mvua zaidi zinatabiriwa mwishoni mwa wiki hii, uharibifu mkubwa unasababishwa na tukio hili baya zidi la hali ya hewa kutokea kwa zaidi ya mwaka mmoja na limehochewa na msimu wa mvua za Monsoon kwenye mwambao wa Bengali.”

Zaidi ya watu 45,000 wameathirika matukio ya mvua hizo za Monsoon zilizoanza tangu mwishoni mwa mwezi Aprili.

WFP imekuwa msitari wa mbele kuwasaidia waathirika kwa misaada mbalimbali na mwezi huu wa Julai limewasaidia wakimbizi 11,000 waathirika wa Monsoon kwa kuwagawia msaada wa chakulakwa ajili ya kendeha familia zao.

Msaada wa WFP kwa Warohingya

Msaada huo wa WFP kwa wakimbizi wa Rohinya walioathirika na mvua za Monsoon unawajumuisha wakimbizi 3,100 ambao wanapokea chakula kilichokwishapikwa na unajumuisha mgao wa wiki moja wa biskuti za kuongeza nguvu ukifuatiwa na mgao wa wiki mbili wa chakula kikavu kama mchele, choriko na mafuta ya kupikia au chakula kilichopikwa.

Bado ni changamoto kubwa kwa watu kutembea kwa miguu au kutumia magari na hata baiskeli kambini hapo kutokana na tope zito lililosababishwa na mvua hizo zinazoendelea ambazo pia zimesababisha mafuriko, na msongamano mkubwa barabarani. Hata hivyo WFP imeweka kituo katika eneo linguine salama la mgao wa chakula kambini hapo na imeweza kusambaza chakula cha msaada ambako kinahitajika zaidi kwenye makambi yote. WFP ina akiba ya kutosha ya chakula kinachoweza kulisha makambi yote Cox’s Bazar ambao ni zaidi ya 900,000 kwa muda wa wiki mbili endapo itahitajika.

Kinachoendelea

Hivi sasa WFP inahaha kukarabati uharibifu mkubwa uliosababishwa na mvua hizo hasa maeneo ya mwunuko ambayo yana utelezi mkubwa na barabara, pamoja na mifumo ya maji safi na maji taka. Wataalam wa WFP ambo ni wahandisi 700  kwa kushirikiana na wakimbizi 3700 wa Rohingya kila siku ndio wanaoendesha ukarabati huo.

Hata hivyo kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa mvua zitaendelea na kuna uwezekano mkubwa wa maporomoko zaidi ya udongo .