Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya sasa ya homa ya Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo

Wahudumu wa afya wakuja kutembelea mama na mwana katika kituo cha matibabu ya Ebola Butembo, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UNICEF/Tremeau
Wahudumu wa afya wakuja kutembelea mama na mwana katika kituo cha matibabu ya Ebola Butembo, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hali ya sasa ya homa ya Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo

Afya

Kuzuka kwa homa ya Ebola katika mikoa ya Kivu Kaskazni na Ituri nchini Jamuri ya Demokrasia ya Congo kumeendelea wiki iliyopita huku maambukizi sawa na hayo yakiongezeka wiki iliyotangulia.

 

Huku idadi ya visa vipya vya homa hiyo ikiendelea kushuka katika maeneo yaliyokuwa yakiathirika sana, kama Butembo, Katwa na maeneo salama kama Mandima, kumekuwa na kuongezeka visa mjini Beni huku visa zaidi vikiripotiwa katika meneo salama ya Mabalako.

Kando na kuibuka maeneo mpya yenye Ebola, kuna idadi kubwa  ya watu waliothibishwa kuugua na wale walioambukizwa wanaoelekea maeneo yaliyo salama, wengi wakitoka eneo la Beni.

Kuhama huku kwa watu waliogua huenda kukasababisha kuenea kwa Ebola kwenda sehemu mpya zilizokuwa salama na pia ugonjwa huo kuibuka maeneo ambapo ulikuwa umedhibitiwa.

Baada ya kuripotiwa kisa cha kwanza eneo lilikuwa salama la Ariwara Juni 30, hakuna kisa kingine tena kimeripotiwa eneo hilo.

Kundi la dharura lililotumwa eneo hilo linaendelea kuchunguza, kushirikiana na jamii na kuwapa chanjo watu walio katika hatari.

Makundi ya dharura kutoka nchi majirani ya Uganda na Sudan Kusini yanaendelea kutoa huduma na kukaa jonjo. Shughuli za kufuatilia hali eneo la mpaka kati ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo inaendelea.

Ndani ya siku 21 kuanzia Juni 19 hadi Julai 9 sehemu 72 zilizo maeneo yenye afya 22 ziliripoti visa vipya, vikiwakilisha asilimia 11 kati ya sehemu 664 zenye afya kwenye mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Pia visa vya Ebola vinazidi kuongezeka miongono wa wahudumu wa afya huku idadi Jumla ya walioambukizwa ikiongezeka hadi 132 ambayo ni asilimia 5 ya visa vyote.