Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 67,000 kuchanjwa dhidi ya surau Ituri DRC-UNICEF

Mama na mwana wapewa chanjo. Chanjo nyingi hutokea baada ya milipuko ya magonjwa  kama vile Polio, Kipindupindu na magonjwa mengine.
UNICEF/ Nangyo
Mama na mwana wapewa chanjo. Chanjo nyingi hutokea baada ya milipuko ya magonjwa kama vile Polio, Kipindupindu na magonjwa mengine.

Watoto 67,000 kuchanjwa dhidi ya surau Ituri DRC-UNICEF

Afya

Wahudumu wa afya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF wanakimbizana na muda katika kampeni ya chanjo kwenye jimbo la ituri Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo baada ya kuzuka mlipuko wa surua uliosababisha karibu vifo 2000 nchi nzima tangu mwanzo wa mwaka huu huku waathirika wengi wakiwa ni watoto wa chini ya miaka mitano.

Kwa mujibu wa UNICEF lengo ni kuchanja Watoto 67,000 jimboni Ituri jimbo ambalo tayari limeathirika na mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini DRC.

Hadi kufikia Juni 23 mwaka huu visa 115,000 vya surau vimeripotiwa iki ni ongezeko karibu mara mbili ya visa 65,000 vya mwaka mzima wa 2018.Afisa wa UNICEF Ituri amesema “Tishio la Ebola na surau kwa maelfu ya familia zinazoishi katika makazi ya wakimbizi wa ndani yaliyofurika ni kubwa mno na tuna fursa ndogo ya kuzuia zahma kubwa ya kupoteza maisha ya watu.”

Chanjo ya kupambana na mlipuko wa suarua inafanyika katika kambi hii ya wakimbizi wa ndani ya Bunia nchini Congo DRC, (Julai 2019)
© UNICEF/Marixie Mercado
Chanjo ya kupambana na mlipuko wa suarua inafanyika katika kambi hii ya wakimbizi wa ndani ya Bunia nchini Congo DRC, (Julai 2019)

Kwa sasa UNICEF inasema chanjo inafanyika katika makazi manne ya wakimbizi wa ndani Bunia Ituri ambako kumeshuhudia wimbi kubwa la familia ziliazolazimika kukimbia mapigano katika wiki za hivi karibuni.

Na kutokana na kuwepo mlipuko wa Ebola eneo hilo uendeshaji wa chanjo lazima uwe wa tahadhari kubwa wahudumu wa afya wanalazimika kuvaa mavazi maalum ya kujinginga na mbali ya chanjo wataendesha pia vipimo kuhakikisha wanaowachanja hawana Ebola.

Jumlaya watu laki nne wanasadikika kuwa wakimbizi wa ndani katika jimbo la Ituri wengi wakiwa wanawake na Watoto wakiishi katika makambi 35 yaliyoko jimboni humo. “Kaskazini Mashariki mwa Congo ni maskani ya moja ya migogoro mibaya zaidi ya kibinadamu leo hii. Ama iwe ni Ebola, surau au hata ukimbizi wa ndani kambini, Watoto wako katika hatari kubwa ya maisha yao. Tunapaswa kufanya kila liwezekanalo kuwalinda” amesema afisa wa UNICEF jimboni humo.