Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UN kuzuru Msumbiji taifa linalojikongoja baada ya vimbunga

Ikiwa ni  miezi mne baada ya Idai, eneo la pwani la mji wa Beira bado linajikwamua na athari za kimbunga hicho
UN Mozambique
Ikiwa ni miezi mne baada ya Idai, eneo la pwani la mji wa Beira bado linajikwamua na athari za kimbunga hicho

Mkuu wa UN kuzuru Msumbiji taifa linalojikongoja baada ya vimbunga

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atazuru Msumbiji Alhamisi na Ijumaa wiki hii wakati ambao taifa hilo la Kusini mwa afrika likijikongoja na ujenzi mpya baada ya kuathirika vibaya na vimbunga Idai na Kenneth vilivyokumba mwezi Machin a aprili 2019. Ujenzi mpya unatarajiwa kugharimu dola bilioni 3.2.

 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kimbunga Idai kiliathiri watu milioni 1.8 katika majimbo ya Inhambane, Manica, Tete, Zambézia na Sofala. Huku katika mji wa Beira pekee asilimia 90% ya miundombinu yote imesambaratishwa.

Na wiki sita tu baadaye wakati watu bado wakihaha kujikwamua na athari zahma nyingine ikawafika, kimbinga Kenenneth ambacho kiliathiri Zaidi majimbo ya Kaskazini ya Cabo Delgado na Nampula, na kuathiri watu Zaidi ya laki 4. Vimbunga vyote viwili vikafuatiwa na mvua kubwa kwa muda wa wiki sita na kuleta balaa ya mafuriko ambayo wakati mmoja mhudumu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa aliyaita “bahari ya nchi kavu” ambayo ilikuwa kubwa kuliko nchi ya Luxembourg.

Ziara ya Katibu Mkuu

Katibu Mkuu, António Guterres, amewasili Msumbiji Alhamisi Julai 11 , ikiwa ni mezi minne baada ya janga la kwanza kubwa la asili nchini humo. Guterres atakutana na Rais Filipe Nyusi,wa nchi hiyo na kupewa taarifa kutoka kwa mashirika mbalimbali ya misaada ya kibinadamu yaliyoko katia maeneo yaliyoathirika na vimbunga hivyo. Mwezi uliopita nchi hilyo ilifanya mkutano wa kimataifa wa kuchangisha fedha kutoka kwa mashirika na wahisani ikitarajia kukusanya dola bilioni 3.2 ili kuwezesha ujenzi mpya katika maeneo athirika. Lakini wahisani wa kimataifa waliahidi dola bilioni 1.2 pekee na kuliacha taifa hilo na upungufu wa dola bilioni 2 kuweza kukamilisha ujenzi mpya.

Katibu Mkuu wa UN António Guterres
UN /Jean-Marc Ferré
Katibu Mkuu wa UN António Guterres

 

Wakati huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema kwamba “Huu ni wakati wa kudhihirisha kwa vitendo mshikamano wetu na taifa ambalo limeathirika na moja ya majanga mabaya Zaidi ya heli ya hewa katika historia ya Afrika.” Kwake yeye janga hilo pia “ni tahadhari kuhusu uharaka wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.”

Mnepo

Katika mji wa pili kwa ukubwa wa Beira nchini Msumbuji moja ya maeneo ambayo atazuru Guterres ni katika shule ya 25 de Junho. Hili ni eneo ambalo watu wengi wanaishi waliotawanywa na vimbunga hivyo , wakilala kwenye madarasa yaliyofurika na kula chakula kinachogawiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake hadi pale watu hao watakapoweza kujenga upya nyumba zao zilizosambaratishwa na kimbunga.

Mkuu wa shule hii ni Frederico Francisco anasema hivi sasa shule hiyo inahifadhi Watoto 5000 wa darasa la kwanza hadi la tisa  na wanasoma kwa awamu tatu kuanzia saa 12 asubuhi wote wakiwa amevalia sare za shule  za rangi ya blu wasichana kwa wavulana wanajaa darasani na darasa moja huchukua wanafunzi 90.Mwalimu Francsco anasema

Shule hii ina madarasa matano tofauti moja lilikamilika mwaka jana na lilijengwa na jamii. Kwa sasa madirisha bado yamebomoka nap aa iliezuliwa na kimbunga na mabaki ya paa hiyo yananing’inia vichwani mwa wanafunzi wakati wakijinzunza hisababi na sayansi chini ya jua kali.

Kurejea kwa maisha

Mratibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya Idai Peter Rodrigues, amesema shirika hilo limewafikia takribani watu milioni 1.6 kwa msaada wa chakula hadi sasa mgao ambao utawafikisha katika msimu ujao wa mazaomwezi Machi 2020 na shirika hilo lina mpango wa kuwasaidia watu wengine karibu laki 6 hadi laki 7 zaidi wasiojiweza kwa gharama ya dola milioni 110.

 

Shule nyingi katika mji wa Beira ziliathirika na kimbunga Idai.
World Bank / Sarah Farhat
Shule nyingi katika mji wa Beira ziliathirika na kimbunga Idai.

Hivi sasa makazi yote ya muda yanafungwa , mjini Beira kuna takriban watu 46,000 wanaoishi katika makambi 15 ambayo ni makazi ya kudumu. Katika maeneo ambayo yameathirika sana na kimbunga cha pili cha Kenneth kuna watu karibu 1300.

Hortênsia Arnaldo Abreu Júlio, mwenye umri wa miaka 26,na wanawawe watatu ni moja ya familia ambazo hazirejei nyumbani.  Aliishi kitongoji cha Mataquari, kwenye viunga vya Beira,lakini nyumba yake ilisambaratishwa kabisa na kimbunga “Sina chochote kilichosalia cha kunifanya nirejee kukifuata.”Kimbunga kilipotokea yeyé na watoto wake ilibidi wapate hifadhi kwenye gari la kaka yake kwa siku kadhaa na baadaye ndipo akaishi kwenye makazi ya muda kwenye shule na kisha kuhamishiwa kwenye moja ya vituo vya jamii.Kwa sasa anasema hana tena mzigo wa kusaka nini watakachokula watoto wake kwani kwenye kituo hiki anapewa angalau mchele kidogo, unga, maharage vitu ambavyo wanaweza kula.

Baadaye alipewa makazi ya kudumu ya kuishji kwenye kambi ya Mutuwa kilometa 40 kutoka Beira yeye akiwa na familia zingine 375. Wanaishi katika mahema waliyopewa na shirika la kuhudumia wakimbizi la UNHCR likishirikiana na lile na wahamiaji la IOM na wadau wengine. Amesema ndoto yake kila siku imekuwa “Kuwa na kipande cha shamba, nililia sana baada ya kimbunga wakati wanangu walipolazimika kulala na watu wasiowagfahamu katika vyumba vilivyofurika . Nilisali sana kwa ajili ya kupata nyumba na kipande cha ardhi mahali ambapo mimi na wanangu tutakuwa salama.”