Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinaenda mrama katika kufikia leongo la elimu 2030:UNESCO

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs  yako 17 .
UN SDGs
Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yako 17 .

Nchi zinaenda mrama katika kufikia leongo la elimu 2030:UNESCO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ikiwa ni takribani miaka mitano tangu Umoja wa Mataifa nan chi wanachama kupitisha malenmgo ya maendeleo endelevu SDG’s yatakayofikia ukomo hapo 2030 makadirio ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO yanaonyesha kwamba nchi zote duniani zitashindwa kutimiza ajenda ya lengo namba 4 la malengo hayo endapo hakutakuwa na hatua za maana zitakazopigwa katika muongo ujao.

Matarajio hayo ya UNESCO kabla ya jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa ambalo litatathimini hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa malengo hayo ya maendeleo, yanaonyesha kwamba wakati Watoto wanastahili kuwa shuleni , mtoto 1 kati ya 6 wa umri hadi wa miaka 17 bado hawatapata elimu ifikapo 2030.

Mambo yatakavyokuwa

Matarajio hayo pia yanaonyesha kwamba asilimi 40 ya watoto kote duniani watashindwa kumaliza elimu ya sekondari idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka na kufikia asilimi 50 Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara ambako idadi ya waalimu waliopata mafunzo muafaka imekuwa ikipungua tangu mwaka 2000.

Matarajio hayo mapya “kutimiza ahadi:je nchi ziko katika mstari wa kufikia SDG 4?” Yametolewa na taasisi ya takwimu na ufuatiliaji wa ripoti ya elimu kimataifa ya UNESCO . Takwimu hizo kwa mujibu wa UNESCO zitatia hofu hasa ukizingatia kwamba lengo namba 4 la maendeleo linahimiza watoto kusoma na sio tu kusajiliwa shuleni.

Athari za takwimu hizo

Katika mwendendo wa sasa makadirio hayo yanasema kiwango cha kusoma kinatarajiwa kudumaa kwa nchi za kipato cha wastani na kushuka kwa takribani theluthi moja kwa nchi za afrika zinazozungumza Kifaransa ifikapo 2030.

Na bila juhudi za kusongesha mbele mchakato asilimia 20 ya vijana na asilimia 30 ya watu wazima katika nchi za kipato cha chini hawataweza kusoma ifikapo mufa wau komo wa kutokomeza ujinga wa kutojua kusoma na kuandika.

Msisitizo wa SDG’s

Ajenda ya maendeleo endelevu yam waka 2030 inasisitiza kusiwe na yeyote atakayeachwa nyumba lakini UNESCO inasema ni asilimia 4 tu ya kati ya asilimia 20 ya watu masikini kote duniani  ndio wanaomaliza elimu ya juu ya sekondari ikilinganishwa na asilimi 36 kwenye nchi tajiri na pengo ni kubwa zaidi katika nchi za kipato cha wastani au cha kati.

Mwaka 2015 UNESCO ilitoa ripoti ya kimataifa ya ufuatiliani wa masuala ya elimu ambayo ilibaini kwamba kwa mwaka kumekuwa na upungufu wa dola bilioni 39 za kuwezesha kufikia lengo namba 4 la SDGs na msaada kwa elimu haujaongezeka tangu mwaka 2010. Mkurugenzi wa taasisi ya takwimu ya UNESCO Silvia Montoya amesema “nchi zinahitaji tawkimu zaidi na zilizo bora ili kulenga sera na kutumia vyema kila senti kuhusu elimu. Takwimu ni lazima na sio ufahari kwa nchi zote. Lakini bad oleo hii chini ya nusu ya nchi zote ndizo zinazoweza kutoa takwimu zinazohitajika katika kufuatilia hatua zilizopigwa kuelekea utimizazi wa lengo la elimu kimataifa.Kuna haja gani ya kuweka malengo ambayo hatuwezi kuyafuatilia, hivyo ufadhili zaidi na uratibu mzuri vinahitajika kuzisaidia nchi, kuziba pengo la takwimu na la muhimu zaidi kupiga hatua zaidi kabla ya kufikia ukomo wa utimizaji wa malengo hayo ya maendeleo.”