Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo kipya cha UNMISS kuleta nuru Kodok Sudan kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamefungua kituo cha operesheni Kodok, jimbo la Fashoda.
UN Photo/Isaac Billy
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamefungua kituo cha operesheni Kodok, jimbo la Fashoda.

Kituo kipya cha UNMISS kuleta nuru Kodok Sudan kusini

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan kusini UNMISS umezindua rasmi kituo chake kipya kwenye eneo la Nile Magharibi  kwa lengo la kuchagiza na kusaidia juhudi za ujenzi wa amani na kuvutia wahudumu wa masuala ya kibinadamu.

Hapa ni katika eneo la Kodok Magharibi mwa mto Nile viongozi wa UNIMISS na wa jimbo la Fashoda wakiwasili kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa ofisi hizo mpya katika eneo lililo na wafungaji na wakulima wengi.

Msimu wa mvua barabara katika eneo hili hazipitiki ni bughdha kwa wakulima na wafanya biashara. Lakini mvua hizo ni muhimu sana kwa kilimo na kujaza mto Nile ambao ni njia mbadala ya wasafiri na wafanyabiashara kuja eneo hili.

Katika miaka sita ya vita vya wenyewe kwa wenyewe Kodok ilitelekezwa na maelfu ya wakazi kufungasha virago, lakini sasa kufuatia muafaka mpya wa amani watu wanaanza kurejrea na kituo hiki kipya cha UNMISS na ukarabati wa barabara huenda vikaleta nuru. David shearer ni mkuu wa UNMISS

(SAUTI YA DAVID SHEARER)

“Ni muhimu sana kwetu kimkakati kuwa hapa. Mosi ni upande wa Maghjaribi wa Nile hivyo ni vugumu kufika kama hatuna kituo hapa. Pili tunachotumai kukifanya ni kwamba kitavutia wahudumu wa kibinadamu katika eneo hili, wataweza kutoa huduma kwa idadi kubwa ya watu ambao wanaanza kurejea, watarejea  Zaidi endapo wataweza kupata huduma kama za elimu, za afya kama hizo, hicho ndicho tunajaribu kufanya.”

Na ili kuweka mazingira salama ya familia zilizotawanywa kuanza kurejerea nyumbani UNMISS ilipeleka walinda amani katika eneo hilo mwaka jana. Na inasema mchakato wa kuanzisha kituo ulikuwa na changamoto nyingi ukizingatia eneo lenyewe liko maporini , na miundombinu ni duni sana.

Sasa baada ya kazi kubwa UNMISS imeshaanza kuona matunda ya kituo hicho na kuboreshwa kwa barabara kwani mamia ya familia zinarejea nyumbani huku chakula na bidhaa zingine vikiwasili Kodok japo haikuwa rahisi

(SAUTI YA DAVID SHEARER)

“Ilikuwa vigumu sana kuweka kituo hapa . wakati wa msimu wa mvua inashindikana kusafiri . Na mara kilipokamilika nadhani wamefanya kazi nzuri, kazi nzuri kwa Umoja wa Mataifa na pia kwa jamii ya hapa.”

TAGS: UNMISS, Kodok, Sudan Kusini, David Shearer, amani