Mazao ya kilimo yanatarajiwa kupunguza bei ya vyakula katika muongo mmoja ujao licha ya hali ya sintofahamu katika siku zijazo-FAO

8 Julai 2019

Mahitaji ya bidhaa za kilimo yanatarajiwa kukua kwa asilimia 15 katika kipindi cha muongo mmoja ujao huku, ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa za kilimo ukitarajiwa kuongezeka kwa kasi zaidi na kusababisha mfumko wa bei. Nayo bei ya bidhaa muhimu za kilimo ikitarajiwa kusalia katika viwango vya sasa au kushuka chini kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo na lile la chakula na kilimo duniani, FAO.

Ripoti hiyo ambayo imewasilishwa mjini Roma, Italia hii leo inatoa utafiti ukilienga mwelekeo wa miaka kumi ijayo katika soko la bidhaa za kilimo na samaki katika viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO, José Graziano da Silva amesema kilimo kimataifa kimebadilika huku operesheni zake zikifanyika katika shamba ndogo hadi kampuni za kimataifa. Aidha amesema kando na kuwasilisha chakula, wakulima wa leo ni muhimu katika kulinda mazingira na wamekuwa wazalishaji wa kawi endelevu.

Bwana da Silva amesema ripoti hiyo inaonyesha pia kwamba“Tutashuhudia ongezeko la matumizi ya vyakula lakinia ukuaji mdogo wa kiuchumi ukijumuishwa na mizozo na mabadiliko ya tabianchi unaathiri uhakika wa chakula na uzalishaji wa bidaha za kilimo, kando na changamoto ya lishe duni, Dunia inakabiliw ana changamoto ya uzito kupindukia na utipwatipwa huku tipoti ikitaja ukuaji wa miji kama sababu kuu ya mabadiliko ya maisha na ulaji.”

FAO imesema kanda zilizo na mahitaji zaidi zinatarajiwa kushuhudia ukuaji wa kiuchumi mdogo na hivyo mabadiliko madogo tu katika lishe yao. Hata hivyo bwana da Silva amesema kuna matumaini kwani

“Kuna utambuzi kwamba sera bora huenda zikasaidia kukabiliana na changamoto zas asa, tunahitaji kuchagiza watumiaji bidhaa kukumbatia lishe bora, wakati huo huo tuanhitaji kutoa msukumo kwa watu walioko sekta ya kilimo ili waweze kuzalisha chakula klicho na ubora."

Ripoti imesema makadirio ya sasa yanaonyesha kupungua kwa ubora wa lishe na kwa hali ya sasa dunia iko hatarini kutofikia ajenda ya mwaka 2030 ya kutokomeza njaa kabisa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud