Mauaji ya bila kukusudia husababisha vifo vingi kuliko mizozo:UNODC

8 Julai 2019

Takriban watu 464,000 kote duniani waliuawa bila kukusudia mwaka 2017, idadi iliyopita kwa mbali ile ya watu 89,000 waliouawa kwenye mizozo na vita katika kipindi kama hicho, kwa mujibu wa utafiti uliofanyika dunia nzima kuhusu mauaji ya bila kukusudia mwaka 2019  na kuchapishwa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusisika na madawa na uhalifu (UNODC). 

“Utafiti wa dunia nzima kuhusu mauaji ya bila kukusudia unaweka wazi suala la mauaji kwa misingi ya kijinsia, yanayotokana na magenge ya uhalifu na changamoto zingine, kusaidia kusaidu kupunguza viwango vya mauaji bila kukuudia,” amesema mkuruenzi mtendaji wa (UNODC) Yury Fedotov.

Fedotov ameendelea kusema nchini zimeahidi viwango vilivyo chini ya maendeleo endelevu kupunguza kila aina ya ghasia na vifo vinavyohusiana na ghasia ifikapo mwaka 2030.

Utafiti huo unaonyesha idadi jumla ya watu waliokumbwa na mauti yaliyotokana na mauaji ya kutokusudia iliongezaka kwa robo ya kwanza ya karne kutoka watu 395,542 mwaka 1992 hadi 464,000 mwaka 2017.

Hata hivyo, sababu kuwa idadi ya watu duniani imeongezeka kwa kasi kuliko ile ya visa vya mauaji yasiyo ya kukusudia, hatari ya kuuliwa bila kukusuadia imeshuka taratibu. Idadi ya watu waliouliwa kwa njia hiyo kwa kila watu 100,000 ilishuka kutoka 7.2 mwaka 1992 hadi 6.1 mwaka 2017.

Uhalifu uliopangwa huchangia asimia 19 ya mauaji yasiyo ya kukusudia

Uhalifu uliopangwa pekee ulichangia hadi asilimia 19 ya mauji yote ya bila kukusudia mwaka 2017. Tangu mwanzo wa karne ya 21, uhalifu uliopangwa ulisababisha vifo vya watu wengi sawa na vifo vinavyotokea kwenye mizozo kote duniani kwa jumla.

Sawa na mizozo, uhalifu uliopangwa hutukiza mataifa, huathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kuhujumu sheria.

Viwango vya mauaji ya bila kukusudia ni tofauti kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Viwango vya mwaka 2017 vya dunia vya mauaji ya bila kukusudia ni tofauti kimaeneo. Viwango katika mataifa ya Amerika vya (17.2) vilikuwa vya juu kurekodiwa eneo hilo tangu kumbukumbu zianze kuwekwa 1990. Viwangi vya Afrika vya (13.0) vilikuwa pia vya juu huku vile vyu Asia, Ulaya na Oceania vikiwa chini vya (2.3, 3.0 na 2.8 mtawalia).

Licha ya viwango ya mauaji ya bila kukusudia kusalia kuwa vya juu katika mataifa ya Amerika, mambo ni tofauti katika kanda hiyo na pia kati ya nchi.

Huko Amerika ya kati nchi yenye viwango vya juu zaidi vya (62.1) ina viwango zaidi ya mara saba ya vile vya nchi iliyo na viwango vya chini zaidi. Marekani Kusini nchi yenye viwangi vya juu zaid vya mauji yasiyo ya kukusudia vya 56.8 ilikuwa na viwango mara 16 zaidi ya nchi yenye viwango vya chini zaidi.

Waathiriwa wengi zaidi wa mauaji yasiyo ya kukusudia ni wanaume, lakini wanawake mara nyingi huuliwa na familia au wapenzi.

Kote duniani asilimia 81 ya waathiriwa wa mauaji yasiyo ya kutarajia vilivyorekodiwa mwaka 2017 walikuwa ni wanaume na watoo wakiume, na zaidi ya asilimia 90 ya washukiwa katika visa hivyo walikuwa na wanaume kwa mujibu wa makadirio ya hivi punde.

Hata hivyo utafiti unaonyesha kuwa tofauti kwa misingi ya jinsia kati ya waathiriwa inabadilika kulingana na umri.

Katika maeneo yote, uwezekano wa wavulana kuwa waathiriwa wa mauaji yasiyo ya kukusudia huongezeka kwa umri licha na visa hivyo kutokea katika umri tofauti. Wanaume na wavulana walio kati ya umri wa miaka 15 na 29 wako katika hatari kubwa kukubwa na mauaji yasiyo ya kukusudia.

Licha ya wanawake na wasichana kuchukua asilimia ya chini ya waathiriwa kwa jumla kuliko wanaume, wanaendelea kukumbwa na mzigo mkubwa wa mauaji kutoka kwa mpenzi au mauaji yanayohusiana na familia.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter