Nchi wanachama wa COMESA na ITCwatangaza ushirikiano wa biasahara

Biashara kama hii ya mjasiriamali huko Zambia anayebadili Chupa ambazo awali zilikuwa taka na kuzifanya mapambo zinaweza kupata wateja duniani kote kutokana na soko la mtandaoni.
UNIC Dar es salaam/Stella Vuzo
Biashara kama hii ya mjasiriamali huko Zambia anayebadili Chupa ambazo awali zilikuwa taka na kuzifanya mapambo zinaweza kupata wateja duniani kote kutokana na soko la mtandaoni.

Nchi wanachama wa COMESA na ITCwatangaza ushirikiano wa biasahara

Ukuaji wa Kiuchumi

Kituo cha kimataifa cha biashara (ITC) na Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika (COMESA)  wametangaza  kuwa watafanya ushirikiano kwa lengo la kuboresha biashara kati ya nchi za Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa ITC Arancha González na Katibu Mkuu wa COMESA Chileshe Mpundu Kapwepwe, Julai mosi mwaka huu walitia saini makubaliano ya kufanya kazi pamoja kubuni na kutekeleza msaada wa kiufundi katika Jumuiya hiyo ya nchi 21.

Pande hizo mbili  zilihaidi kushirikiana katika nyanja kama vile umoja wa masoko, ukuaji wa viwanda, ushindani wa biashara na kuboresha zaidi biashara ya kanda na mitandao ya uwekezaji. Pande hizo mbili zitatilia maanani kwa kiwango fulani suala la kuwainua wanawake na vijana kwa njia ya biashara.

‘Muingiliano kamili wa kikanda utahitaji ushindani wenye nguvu na wa kuzalisha baina ya nchi wanachama kuongeza biashara kati ya Jumuia ya (COMESA) na dunia,’ alisema Katibu Mkuu wa COMESA Chileshe Mpundu Kapwepwe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ITC ambacho ni kitengo tanzu cha Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD amesema ‘kuongezeka kwa biashara kati ya nchi za Afrika inakuwa  na umuhimu katika ukuaji wa nchi za Afrika, .

Bi. Gonzales ameongeza kuwa  ‘kufuatia kuja kwa makubaliano kama yale ya biashara huru ya bara la Afrika  (AfCFTA), mashirika kama (COMESA ) yana wajibu mkubwa wa kuhakikisha mafanikio yao. Hapa (ITC) tuna furaha kuongeza ushirikiano na (COMESA) na kuhakikisha ushindani zaidi kati ya nchi wanachama.’

Kulingana na malengo ya mashirika yote mawili ya kuhakisha kuwepo kwa fursa kwa biashara ndogo, ITC na (COMESA) wataongeza jitihada za kuhakikisha kuwepo kwa mazingira ya biasha kwenye nchi wanachama na kuongeza  misaada kwa mashirika na mitandao ya biashara za wanawake.