IAEA yaisaidia Msumbiji kukabiliana na maradhi ya mifugo baada ya mafuriko:

2 Julai 2019

Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA, limepeleka vifaa vya dharura ili kuisaidia Msumbiji kupambana na mgonjwa ya mifugo kama homa ya Afrika ya nguruwe, ugonjwa wa miguu na midomo  au homa ya bonde la ufa magonjwa ambayo yanaweza kuleta athari kubwa na kutishia mustakabali wa mifugo na binadamu baada ya mafuriko yaliyosababishwa na vimbunga vya hivi karibuni.

Msaada huo wa IAEA umepelekwa kwa ombi maalumu la wizara ya kilimo na uhakika wa chakula ya Msumbiji. Msaada uliotolewa na IAEA unajumuisha vifaa vya maabdara, utaalam wa kiufundi, na mamia ya dawa za kemikali  ambazo zitasaidia kufanya uchunguzi na vipimo vya mapema , lakini pia upimaji wa kutumia nyuklia na kufuatilia magonjwa hayo kwenye maeneo ambayo yameathirika zaidi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya amano nchi hiyo ya Kusini mwa afrika ili kubwa na vimbunga viwili vikubwa hivi karibuni vilivyosababisha mafuriko yaliyoisambaratisha pia mashamba. Mbali ya kukatili maisha ya watu wanyama zaidi ya 300,000 waliuawa na wengine milioni 6 kuwekwa katika hatari kubwa ya maradhi.Ameongeza kuwa msaada wa haraka wa IAEA unaisaidia Msumbiji kujiandaa na uwezekano wa mlipuko wa magonjwa ya mifugo. “watu mara nyingi kuwaodoa wanyama katika maeneo ya majanga hivyo huchanganyika zaidi na mlipuko wa magonjwa unaweza kuzuka.” Amesema Herman Unger daktari wa mifungo na afisa wa kiufundi wa kitenngo cha pamoja cha utaalam wa nyuklia katika chakula na kilimo wa IAEA na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO“Endapo na maelfu ya mifugo pamoja unachohitaji tu kuzuka magonjwa ni mnyama mmoja kuugua.”

Msaada wa IAEA utasaidia kufanya uchunguzi kwa kutumia teknolojia ya nyuklia ili kubaini magonjwa haraka na kwa uhakika zaidi. Na uchunguzi wa mapema ni muhimu katika kudhibiti kusambaa kwa magonjwa ya mifugo na kuyatibu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kuwatenga mifugo wagonjwa na pia kuendesha kampeni.

Msaada huo utatilia mkazo uchunguzi wa magonjwa kama homa ya bonde la ufa inayoenezwa na mbu na ambayo inaweza kuambukizwa kwa binadamu pia . Magonjwa mengine yatakayofanyiwa uchunguzi na vipimo ni ugonjwa wa muguu na midomo, ugonjwa wa Newcastle, mafua ya avian na PPR.

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter