Tunachokipigania Tanzania sio idadi tu bali pia ubora wa wanawake viongozi: Ummy Mwalimu

2 Julai 2019

Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika harakati za ukombozi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali iikiwemo kijamii, kiuchumi na hata kisiasa. Flora Nducha na tarifa zaidi

Kwa mujibu wa waziri wa maendeleo ya jamii , jinsia wanawake, wazee na watoto wa Tanzania Ummy Mwalimu wanawake nchini Tanzania wameanza kutambua thamani yao na nafasi yao katika jamiiikiwemo masuala ya uongozi, mathalani amesema  bugeni sasa wana uwakilishi wa wanawake aslimia 37 lakini la msingi zaidi si idadi bali ubora na mchango wao na hasa katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu inayosisitiza kutomwacha yeyote nyuma.

Akifafanua zaidi kuhusu hoja hiyo alipozungumza nami waziri Ummy amesema "kwangu mimi kama waziri ambaye nashughulikia maswala ya wanawake, sio idadi lakini pia je tunpata ubora wa uwakilishi, tunazisikia sauti za asilimia 37 za wanawake?"

Na je matunda yameanza kuonekana? Bi Mwalimu amesema, "wabunge  wanawake kwa kweli wamekuwa wakifanya kazi nzuri inapokuja mijadala na kupitisha sheria unaona wanakuwa makini. Hapa tunatakuja kuona usawa wa kijinsia na ushiriki wa wanawake ukizungumziwa, kwa hiyo unakuta hata sheria tunapopitishia bungeni zinazingatia  maswala ya wanawake. Lakini hata michango  ya wabunge wanawake bungeni, wabunge wanawake utasikia wanaongea kuhusu afya, kwenye mambo ya maji utawakuta kwenye mambo ya kilimo, kwasababu asilimia 60 ya wazalishaji wa chakula cha nyumbani utakuta ni wanawake. Kwahiyo utakuta kuwa wabunge wanawake wanakuwa wakali sana kwenye  mawala ambayo yanawagusa wanawake moja kwa moja."

Kwa mafanikio hayo kwa Waziri Ummy anasema, "kwangu mimi kwa kweli nafurahi kwamba sio tu kwamba tumeongeza idadi ya wabunge wanawake lakini pia tumeongeza mchangu mkubwa sana wa wanawake katika masuala ya maendeleo."

 

 

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter