Wahudumu wa afya na serikali Uganda wanafanya kazi nzuri kudhibiti Ebola:WHO

28 Juni 2019

Shirika la afya ulimwenguni WHO limewapongeza wahudumu wa afya na wizara ya afya ya Uganda kwa hatua za haraka na maandalizi ya kupambana na mlipuko wa Ebola uliozuka hivi karibuni nchini humo. 

Hapa ni katika hospitali ya Bwere katika eneo lililo katika hatari ya Ebola mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Uganda  ambako mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa WHO Matshido Moeti ametoa pongezi hizo baada ya kutathimini hali ya ebola katika eneo hilo.

(SAUTI YA DKT MOETI )

“kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika maandalizi , na hatua hizo zimewezesha kujenga uwezo, kushirikiana na wadau wengi, na mambo yoye ya muhimu yanayohitajika yamewekwa tayari hapa. Na inaonekana kwamba hatujashuhudia ongezeko la visa hivyo tunamatumaini kwamba hatua hizi zinafanya kazi.”

Uganda ilitangaza mlipuko wa Ebola Juni 11 mwaka huu na tangu wakati huo visa vitatu ndio vilivyothibitishwa na wote walitokea nchi jirani ya DRC. Moja ya tahadhari kubwa inayochukuliwa ni chanjo

(SAUTI YA DKT MOETI)

“Tunashukuru kila uwekezaji uliowekwa kuhakikisha mfumo unafanya kazi kukabiliana na wagonjwa wakijitokeza. Na tunaweza tu kuahidi kuendelea kusaidia hadi pale hatari itakapokwisha upande wa pili wa mpka DRC. Kwa sababu ni lazima tuendelee na hatua hizi, timu hii kuwa tayari endapo kutakuwa na mtu atakayehitaji matibabu.”

Kati za ziara hiyo wilayani Kasese Bi . Moeti ameambatana na waziri wa afya wa Uganda Dkt. Jane Ruth Aceng ambaye ameishukuru WHO kwa msaada wa maandalizi ya kukabiliana na mlipuko Uganda na pia katika kupambana na visa vilivyozuka. Ingawa kwas asa hakuna visa vipya vya ebola waziri Aceng anasema bado wanachukua tahadhari

(SAUTI YA DKT JANE ACENG)

“Hata kama hatuna kisa chochote cha ebola Uganda , hata kama hatuna tena washukuwa wa visa hivyo bado tutakuwa katika hali ya tahadhari kwa sababu tayari tulishakuwa na visa vilivyothibitishwa vya Ebola nchini na hatuwezi kutangaza kwamba mlipuko umekwisha kwa sababu kuna uwezekano wa mlipuko huo bado katika upande wa pili.”

Katika ziara hiyo ya siku mbili Dkt Moetoi alifika hospital ya Bwera ambako watu wawili waliokuwa na Ebola kati ya visa vitatu vilivyothibitishwa walitoka.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter