Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kwanza wa uchumi na wanyamapori Afrika wafanyika Zimbabwe:UNEP

Kati ya mwaka 2010 na 2012, tembo 100,000 waliuawa barani Afrika kwa ajili ya meno yao.
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch
Kati ya mwaka 2010 na 2012, tembo 100,000 waliuawa barani Afrika kwa ajili ya meno yao.

Mkutano wa kwanza wa uchumi na wanyamapori Afrika wafanyika Zimbabwe:UNEP

Ukuaji wa Kiuchumi

Wakuu wanne wa nchi wamekutana katika mkutano wa kwanza kabisa kuwahi kufanyika Afrika kuhusu uchumi na masuala ya wanyamapori.

Kwa mujibu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP mkutano huo unaofanyika Victoria Falls nchini Zimbabwe una lengo la kuweka masuala ya wanyama pori katika kitovu cha maendeleo ya koiuchumi na watu. 

Kwa pamoja wakuu hao w anchi kutoka Kusini mwa afrika , jamii na sekta binafsi wamejadili jinsi gani ya kujenga uchumi endelevu utokanao na wanyama pori.

Akizungumza katika mkutano huo kaimu mkurugenzi mtendaji wa UNEp Joyce Msuya amesema “kwa mara ya kwanza barani Afrika tunawaweka wanyama pori katika kitovu cha maendeleo ya kiuchumi na watu”.

Ameongeza kuwa hivi sasa kuna aina nyingo ya viumbe ambao wako hatarini kutoweka kutokana na kumomonyoka kwa maliasili, na mgogoro baina ya binadamu na wanyama pori.

Mwa mantiki hiyo wawakilishi kutoka jamii zaidi ya 40 wameamua kuandaa azimio linalotoa wito wa kuwa na makubaliano mapya na jamii za asili zilizoko katika maeneo ya uhifadhi. Bi. Msuya amesisitiza kuwa kwa minajili hiyo “watu ni lazima wawe nguzo katika uchumi utokanao na wanyama pori. Hebu tosonge mbele kwa pamoja katika mwelekeo mmoja , kwani kila mmoja ana jukumu la kufanya katika hili”.

Watu mbalimbali wanashiriki mkutano huo wakiwakilisha serikali, jamiaa, asasi za kiraia, sekta za umma na sekta binafsi, wadai wa ulinzi wa wanyama pori na umoja wa Mataifa mkutano huo wa siku tatu unakunja jamvi kesho Ijumaa.