Uhuru wa maoni ni haki ya msingi ya kibinadamu, waliomuua Bilal Khan wawajibike-UNESCO

26 Juni 2019

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Audrey Azoulay ametoa wito kwa mamlaka nchini Pakistan kuwafikisha katika mkono wa sheria waliomuua mwanablogu na mwanaharakati wa kupitia mitandao ya kijamii, Muhamad Bilal Khan.

Bi. Azoulay amesema, “ninalaani mauaji ya Khan. Ninatoa wito kwa mamlaka kuchunguza uhalifu huu na kuwafikisha mahakamani walioutekeleza. Uhuru wa maoni ni haki ya msingi ya binadamu na inatakiwa kutunzwa na kila mtu bila kujali dini au maoni ya kisiasa ya mtu.”

Mnamo tarehe 16 ya mwezi huu wa Juni, washambuliaji wasiofahamika walimuua mwanablogu wa kidini Khan aliyekuwa na umri wa miaka 22 ambaye pia alikuwa mwanaharakati kupitia mitandano ya kijamii.

UNESCO imekuwa ikihamasisha usalama wa wanahabari kupitia katika kukuza uelewa kuhusu haki za wanahabari na pia kukuza uwezo wa wanahabari kote ulimwenguni.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud