Kufa maji kwa baba na mwana toka el salvador hakustahili :UNHCR

Hali halisi inavyokuwa baada ya wasaka hifadhi na wahamiaji kuokolewa na boti za uokozi
UNHCR/Giuseppe Carotenuto
Hali halisi inavyokuwa baada ya wasaka hifadhi na wahamiaji kuokolewa na boti za uokozi

Kufa maji kwa baba na mwana toka el salvador hakustahili :UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na kustushwa kuona picha za maiti ya baba na mwana wakimbizi waliokufa maji kwenye ukingo wa Rio Grande

Kwa mujibu wa shirika hilo ingawa taarifa zaidi za masa huu bado zinakusanywa lakini ni dhahiri mazingira ya kufa maji kwa Oscar Alberto Martinez Ramires na binti yake wa miezi 23 Valeria kutoka nchini Salvador hayakubaliki.

Picha ya maiti hizo zinazoonekana kwenye ufukwe wa Rio Grande UNHCR inasema ni kumbusho ya kilichoshuhudiwa dunia nzima karibu miaka minne iliyopita picha ya maiti yam toto mkimbizi kutoka Syria, alan Kurdi ikiwa imelala kwenye ufukwe wa bahari ya Mediterranea baada ya kufa maji.

Sasa kwa mara nyingine tunakabiliwa na hali halisi kama ile ambayo ni ushahidi wa watu kufa wakati wakiwa katika safari za hatari kujaribu kuvuka mpaka kwenda kusaka usalama na mustakabali bora.

Akizungumzia zahma hiyo Kamisha mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi amesema “Vifo vya Oscar na Valeria hali halisi ya kushindwa kushughulikia machafuko na mazingira yanayowalazimisha watu kuchukua safari hizo za hatari kwa matarajio ya kwenda kusaka Maisha salama nay a utu. Hii inachangoiwa na kutokuwepo na njia salama za watu kutafuta ulinzi, na hivyo kuwaacha wengi kutokuwa na chaguo lolote Zaidi ya kuhatarisha Maisha yao.”

UNHCR imeendelea kutoa wito kwa nchi katika kanda ya Amerika kuchukua hatua za pamoja na mara moja ili kuzuia janga linguine kama hilo kutokea. Pia shirika hilo la wakimbizi limependekeza njia za kuimarisha na kuboresha mchakato wa waomba hifadhi nchini Marekani ikiwemo hali ya mazingira ya mahabusu.

Na Bwana Grandi amesema “Tuko tayari kuzisaidia serikali zote katika kanda hiyo kuhakikisha kwamba mtu yeyote anayehitaji ulinzi wa kimataifa anaupata kwa haraka na bila vikwazo.”

 

TAGS:UNHCR, El salvador, Filippo Grandi, wakimbizi