Lazima tuhakikishw wajane hawaachwi nyuma:UN

Katika siku ya kimataifa ya wajane inayoadhimishwa leo Juni 23 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemtaka kila mtu kutafakari “changamoto za kiuchumi na matatizo wanayopitia wajane na kuhakikisha kwamba hawaachwi nyuma.
Katika ujumbe wake maalum wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Katika kukosekana ulinzi wa kijamii na kisheria katika maisha yao yotemapato na akiba ya wajane mara nyingi ni ndogo
kuweza kuepuka umasikini
Guterres amesema katika nchi nyingi wanajane hawana haki za kurithi kama wanaume, hii ikimaanisha kwamba wanaweza kunyang’anywa ardhi na vitu, na hata haki na fursa za kuwa na watoto wao. Hata katika sehemu ambazo sheria haibagui, haki hizo zinapaswa kutekelezwa na kutumia sawa
ili watu wote wazifurahie.”
Ameongeza kuwa zaidi ya hayo katika baadhi ya jamii wajane hutengwa, kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili ikiwemo ukatili wa kingono,
kudhalilishwa na kuingizwa katika ndoa za shuruti. Guterres pia amezungumzia hali inayowakabili wajane katika migogoro na majanga ya asili ambayo yanaongeza madhila kutokana na
kupoteza kila kitu na kutawanywa ,lakini pia kudhoofisha ulinzi wa kijamii na kisheria , akisistiza kwamba ‘mila zinazotumika kuhalalisha
vitendo hivi vya kibaguzi ni lazima zishughulikiwe.
“Amesema “Katika siku hii ya kimataifa hebu na tudumishe nia yetu ya kuwasaidia wajane wote bila kujali umri, mahali
waliko au mfumo wa kisheria ili kuhakikisha kwamba hawaachwi nyuma."
Kwa upande wake mkurugenzi mtendani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women amesema wakati familia zikidumisha utamaduni na uchumi na kuonyesha upendo na msaada wa kujikimu kwa wanawake hawa ,
mara nyingi kuna sehemu zingine ambako ukatili na ubaguzi kwa wanawake na wasichana vinaendelea na wajane ndio waathirika
wakubwa huku wakikosa msaada.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo Ngcuka katika ujumbe wake wa siku hii ameongeza kuwa”wakati thamani ya mwanamke inaonekana akiwa na mume, ujane
unaweza kumlazimisha mwanamke kutoka nje ya mfumo wa familia au kabila na kumuacha katika hali ya kutojiweza akikabiliwa na
changamoto nyingi kama umasikini, upweke na kutengwa.”
Ameongeza kuwa wanawake masikini mara nyingu husalia wajane kwa sababu ya pengo la umri na wenza katika kaya masikini, kwa kiasi kikubwa ikichangiwa na mila za ndoa za utotoni na umri mdogo wa watu kuishi kwa wanaume masikini, na pia wanawake wajane hukabiliwa na changamoto za kiuchumia kutokana
na mila na sheria kama za kutoweza kurithi. Wakati takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kwamba asilimia 14.6 ya wanawake wa umri wa miaka 55 hadi 59 duniani kote ni wajane , hii sio hali halisi kwa mujibu wa UN women.
Wajane wanaweza pia kuwa mabi harusi watoto ambao waume zao wamefariki dunia na kuwaachia kitu kidogo au bila chochote, bila urithi au fursa za maisha.
Bi Ngcuka amesema “katika siku hii ya wajane tuanawakumbuka wajane wote na kutambua haja ya kuwashirikisha kikamilifu katika kazi zetu
za usawa wa kijinsia ili tuweze kuvunja mzunguko wa umasikini kutokuwa na fursa kwa wajane wote ili kuweza kufurahia haki za binadamu.