Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huu ni wakati wa mabadiliko kwa vijana:Guterres Lisbon+2

Mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana mwaka 2019 na jukwaa la vijana Lisbon+21, mjini Lisbon Ureno. Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihutubia
Lisboa +21
Mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana mwaka 2019 na jukwaa la vijana Lisbon+21, mjini Lisbon Ureno. Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihutubia

Huu ni wakati wa mabadiliko kwa vijana:Guterres Lisbon+2

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa mabadiliko , na kizazi chacke kimeanza kuelewa kwamba vijana wanaweza na wanapaswa kushika usukani .

Guterres ameyasema hayo Jumapili mjini Lisbon Ureno katika hotuba yake ya kufunga mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana wa mwaka 2019 mkutano ambao ni jukwaa la Lisbon+21.  Katika jukwaa hilo la siku mbili amesisitiza kuwa “huu ni wakati wa mabadiliko ya jinsi gani Umoja wa Mataifa unashughulikia masuala ya vijana.”

Mabadiliko

Guterres amesema “Umoja wa Mataifa ulianzishwa katika wakati tofauti sana na sasa na kwamba una mfumo ambao kwa kawaida ni mgumu kubadilika , lakini hilo lazima libadilike. Ameuambia mkutano huo kwamba “tunahitaji kufanya kazi na nyie kuhusu fursa za elimu na afya , kuhusu masualaya ajira na mafunzo, kuhusu haki za binadamu na jinsi ya kuchagiza ushirika kikamilivu wa vijana katia mchakato wa kufanya maamuzi katika masuala haya kuanzia ngazi ya mashinani, kitaifa na kimataifa.”

 

Mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana mwaka 2019 na jukwaa la vijana Lisbon+21, mjini Lisbon Ureno.
Lisboa +21
Mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana mwaka 2019 na jukwaa la vijana Lisbon+21, mjini Lisbon Ureno.

Akiunga mkono kazi kubwa inayofanywa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Vijana Jayathma Wikramanayake Katibu Mkuu amemchagiza “kuendelea kuweka malengo na kupima ukomo wake” na kusema “nategemea uongozi wako na msaada wako.”

Fursa

Katibu Mkuu pia amekumbusha azimio la Lisbon kuhusu sera na mipango ya vijana . Mwezi August mwaka 1998 katika mkesha wa kuelekea karne ya 21 kuliwekwa malengo kadhaa kuhusu sera za vijana. Amesema hatua hiyo ilipelekea mkutano wa kwanza wa mawaziri wanaohusika na masuala ya vijana ulioandaliwa na serikali ya Ureno kwa kushirikiana na wadau wengine kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Ameongeza kuwa “Miaka 21 iliyopita hapa Lisbon nilipata fursa ya kuhutubia mkutano wa kwanza wa mawaziri wa masuala ya vijana. Ni kwa heshima kubwa kwamba leo nimerejea tena kwenye mji huu na jukwaa hiliambapo naona sura nyingi ambazo si ngeni na pia washiriki wengi wapya . Katika miaka hii 21 tumetoka mbali na kupiga hatua kwa pamoja.”

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema “mwaka 1998 intaneti ilikuwa ndio inachukua hatua za awali na majina kama drone na picha za kujipiga au selfi hazikuwepo kwenye kamusi ya maneno yetu ya kila siku. Hatari ya mabadiliko ya tabianchi haikuwa inaeleweka kama sasa na watu waliokuwa wakiishi kwenye umasiki sasa idadi yao imeongezeka mara mbili. Idadi ya wasichana wasiokuwa na fursa ya elimu ya msingi ilikuwa ni ya juu mara mbili ya sasa.”

Akilinganisha takwimu na miaka 21 iliyopita Guterres amesema “kuna watu bilioni mbili vijana wanaoishi kwenye dunia hii sasa, hii ikimaanisha kwamba hiki ni kizazi ha idadi kubwa ya vijana katika historia.

 

Mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana mwaka 2019 na jukwaa la vijana Lisbon+21, mjini Lisbon Ureno. Jayathma Wickramanayake mjumbe wa UN kuhusu vijana akihutubia jukwaa hilo
Lisboa +21
Mkutano wa kimataifa wa mawaziri wa vijana mwaka 2019 na jukwaa la vijana Lisbon+21, mjini Lisbon Ureno. Jayathma Wickramanayake mjumbe wa UN kuhusu vijana akihutubia jukwaa hilo

Changamoto

Guterres amesema hata hivyo kizazi hiki kinakabiliwa na changamoto nyingo na kubwa moja ya tano ya vijana wote hawana ajira, hawakusoma au hawana mafunzo yoyote, robo yao wameathirika na mahafuko au vita na mamilioni ya wasicha wanakuwa kina mama kabla ya wakati wangali bado Watoto.Pia masuala kama uonevu kwenye mitandao na unyanyasaji vinaongeza kiwanngo cha shinikizo na takribani barubaru 67,000wanapoteza maisha kwa kujiua na kujiumiza kila mwaka.

Katibu Mkuu amesisitiza kwamba “Bila kuchukua hatua sasa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kutokuwepo usawa na kutovumiliana kizazi hili kitakabiliwa na athari kubwa.”

Hata hivyo ameongeza kuwa “Kizazi hiki kimeanza kuelewa kwamba vijana wanaweza na wanapaswa kuongeza, ni lazima kuweka mazingira bora kwa vijana mahali ambapo wanahisi hakuna ulinzi, lakini kama raia wenye haki sawa, sauti sawa na ushawishi sawa kama wajumbe kamili wa jamii zetu na mabalozi wenye nguvu ya kuleta mabadiliko.”

Uongozi

Guterres amewashukuru vijana kwa uongozi waliouonyesha katika Nyanja mbalimbali na kuahidi kwamba “Umoja wa Mataifa utakuwa pamoja nanyi wkati wowote mtakaokabiliwa na kukosa haki”.Ameongeza kuwa atafanya kazi na vijana kuzuia migogoro na kuchagiza amani na pia kuunga mkono fursa za elimu, ajira zenye hadhi, ustawi wa jamii na masuala ya afya ya uzazi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu “ushirika huu umejumuishwa katika mkakati wa vijana wa 2030 uliozinduliwa mwaka jana kwa lengo kufanya Umoja wa Mataifa kuwa kiongozi wa kufanyakazi na kushikiana na vijana.