Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nzige na Parara ndio chakula cha siku zijazo- Chef Ali

Hapa ni kwenye moja ya soko nchini Thailand, wadudu wakiuzwa kama kitoweo.
P.B. Durst
Hapa ni kwenye moja ya soko nchini Thailand, wadudu wakiuzwa kama kitoweo.

Nzige na Parara ndio chakula cha siku zijazo- Chef Ali

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo FAO, limeanzisha kampeni ya kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuna uendelevu katika uzalishaji na ulaji wa chakula.

Lengo la kampeni hii iliyopatiwa jina #Actnow au chukua hatua sasa kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la watu duniani, inasaka kuhakikisha kuwa chakula kilichopo au kitakachozalishwa siyo tu kitatosheleza mahitaij  ya kizazi cha sasa na kijacho bali pia kitakuwa ni chakula salama kwa afya ya mlaji.

Kupitia kampeni hiyo,  FAO imeungana na wapishi wakuu kutoka maeneo mbalimbali duniani ikiwemo nchini Kenya. Kutoka Kenya ni mpishi mkuu Ali Mandhry mzaliwa wa Mombasa ambaye amesema tangu mdogo amependa upishi.

Akijulikana zaidi kama Chef Ali, yeye amechukua hatua zaidi na kusaidia watu kufahamu kile kitakachokuwa chakula cha siku za usoni kama alivyozungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.