Michezo haichagui wala kubagua mkimbizi:Nshimirimana mkimbizi wa Burundi

21 Juni 2019

Michezo ni jukwaa ambalo hukutanisha, huunganisha na kuwaleta pamoja watu licha rangi, jinsia au hata watokako na hali zao za maisha. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa michezo ni daraja la amani na wanaichagiza katika maeneo yenye mizozo kwa ajili ya nguvu yale. Na leo inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kukutana na timu ya wasichana watupu wakimbizi toka Burundi wanaosakata kabumbu.

Kutana na timu ya Morning star au nyoota ya asubuhi , walikimbia machafuko Burundi mwaka 2015 na kuhamia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , wakiwa ukimbizini walibaini mapenzi yao ya kusakata kambumbu, wote wakiishi katika kambi ya wakimbizi ya Lusenda. Kapteni wa timu hiyo ni Emarance Nshimirimana na mchezaji mwenzie ni Speciose Nibigira

SAUTI YA NSHIMIRIMANA NA NIBIGIRA

Licha ya kutokuwa na uwanja maalum wa mpira wa miguu, viatu au njumu za kucheza mpira au hata mpira wao wenyewe hawaruhusu chochote kuingilia kati ndoto zao za kuwa wachezaji nyota siku moja

SAUTI MCHEZAJI 1

Nshimirimana anaongeza

SAUTI NSHIMIRIMANA 

Nami nawatakia kila la heri

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter