Idadi kubwa ya watu wanaotawanywa inaonesha tunaeleka kushindwa kuleta amani duniani-Filippo Grandi

19 Juni 2019

Takwimu zinaonesha kwamba mwaka 2018 watu milioni 70 walikimbia vita, mateso na migogoro, amesema hii leo mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR

Bwana Fillipo Grandi ameyaeleza hayo katika kuisihii jumuiya ya kimataifa kuja pamoja kukabiliana na ukweli kuwa, “tunakaribia kushindwa kudumisha amani.”

Akiweka wazi tawkimu  mpya zinazoonesha kuwa idadi ya watu wanaotawanywa ziko katika kiwango cha juu ambacho UNHCR imeshuhudia katika takribani miaka 70 ya uwepo wa shirika hilo, Bwana Grandi amesema haya ni makadirio ambayo ni ya chini ikilinganishwa na hali halisi. 

Hii ni kwa sababu nusu milioni pekee ya Wavenezuela wameomba hifadhi na hadhi ya ukimbizi kati ya watu milioni nne ambao wameihama nchi yao iliyoko matatizoni kutokana na mgogoro wa kiuchumi na kisiasa.

Pia ni kutokana na nchi jirani ya Peru baada ya kulemewa na wahamiaji na hivyo  kuweka masharti zaidi dhidi ya Wavenezuela wanaojaribu kuvuka mpaka wao, Bwana Grandi amesema hatari ni kuwa nchi nyingine zilizoko karibu na Venezuela kama vile Ecuador na Colombia zinaweza kufuata mkondo huo.

“Hawa ni watu ambao wanakimbia kwa hivyo ni vigumu kwao kupata nyaraka kutoka katika nchi zao. Peru ni ya pili kwa ukubwa wa kupkea wakimbizi kutoka Venezuela baada ya Colombia na kwa kweli wameelemewa na uwepo wa watu wote hawa na nasikitika nao lakinitumekuwa tukiwasihi kuwa kama Colombia na Ecuador na Brazil kuiacha mipaka yao wazi kwani hawa watu kwa hakika wako katika uhitaji wa uslama, ulinzi na mengine. Ninatambua kuwa tunawaomba mambo mengi lakini lakini ni kazi yangu kuziomba nchi hizo kuiacha wazi mipaka” Bwana Grandi amewaeleza wanahabari.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNHCR kuhusu mienendo ya dunia, kiwango cha watu kutawanywa ni mara mbili ya ilivyokuwa miaka 20 iliyopita.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter