Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuruhusu kauli za chuki ni kushambulia moja kwa moja maadili yetu:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
TASS/ UN DPI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Kuruhusu kauli za chuki ni kushambulia moja kwa moja maadili yetu:UN

Amani na Usalama

Kauli za chuki ni shambulio la moja kwa moja juu la maadili yetu ya msingi ya uvumilivu, ujumuishwaji na kuheshimu haki za binadamu. Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa uzinduzi wa mkakati na mpango wa kuchukua hatua dhidi ya kauli za chuki kwenye kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.

Guterres amesema Chuki inafarakanisha makundi, huchangia vurugu na migogoro, na hudhoofisha jitihada zetu zote za amani, utulivu na maendeleo endelevu. Kwa hivyo, kushughulikia hilo ni kipaumbele kwa mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa.”

Amesema duniani kote tunashuhudia kutapakaa kwa vitendo vya chuki dhidi ya wageni, ubaguzi wa rangi na kutovumiliana, vurugu za kiitikadi, chuki dhidi ya Uyahudi na chuki dhidi ya Uiislamu.

Katika baadhi ya sehemu ulimwenguni, jumuiya za Kikristo zinashambuliwa. Wakati hotuba za chuki zimekuwepo, kipengele kipya leo ni mawasiliano ya kidigital na hususan, majukwaa ya mitandao ya kijamii.

“Hii inafanya hotuba za chuki kuwa mbaya zaidi kuliko hapo awali, kuimarisha na kuiwezesha kwenda mbali zaidi na kwa kasi.”

Guterres ameongeza kuwa maudhui yaliyojaa chuki yanafikia wafuasi wapya kwa kasi ya umeme, na zimehusishwa na vurugu na mauaji kutoka Sri Lanka hadi New Zealand na Marekani. Pia hutumiwa na vikundi vya ukatili kuajiri na kushawishi watu kuingia katika itikadi kali mtandaoni.

Athari katika jamii

Viongozi wa kisiasa katika baadhi ya nchi wanafuata hotuba hizo na mitazamo ya makundi haya, huwadhuru wale walioathiriwa na kudhoofisha viwango vya ut una hadhi ambayo tumekuwa mayo katika jamii kwa miongo kadhaa.

Katibu mkuu amesema yote haya yakiendelea Umoja wa Mataifa, serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia, wanazuoni na jumuiya ya kimataifa tunapaswa kuongeza juhudi na hatua zetu na hi indio sababu iliyonifanya nikamwambia mshauri maalum kwa ajili ya kuzuia mauaji ya kimbari Adama Dieng, kuandaa mkakati na mpangi ambao tunauzindua leo.

Lengo la mkakati huo

Guterres amesema “lengo la mkakati huu ni kuratibu juhudi zetu kwenye mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa, kushughulikia mizizi ya kauli za  chuki na kuhakikisha hatua zetu kufanya kazi zaidi.”

Ameongeza kuwa mkakati huo unajumuisha hatua kwa ajili ya ofisi za Umoja wa Mataifa makao makuu na zilizoko mashinani katika ngazi ya kitaifa na kimataifa. Na mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yametakiwa kuandaa mipango na mikakati yao wakishirikiana na Adama dieng.

Masuala muhimu katika hatua hizo

Guterres baada ya hotuba yake amezungumza na waandishi wa Habari na kuwaeleza kwamba kuna kitu kimoja ambacho ni muhimu sana “hatua zote zinazotakiwa kushughulikia na kukabiliana na haotuba za chuki zinapaswa kuwa endelevu na zinazozingatia misingi ya haki za binadamu.Umoja wa Mataifa unaunga mkono uhuru wa kujieleza na maoni kila mahali.”

Na kusisitiza kuwa “ kushughulikia kauli za chuki hakumaanishi kuzuia au kubinya uhuru wa kujieleza, kuna maanisha kuhakikisha hotuza za chuki haziendelei na kuwa kitu cha hatari zaidi hususan kuchochea ubaguzi, ukatili na machafuko ambayo yanapingwa chini ya sheria za kimataifa.”

Ametoa wito kwamba “tunahitaji kuchukulia hituba za chuki kama tunavyochukulia vitenfdo vyovyote vibaya: kwa kuzilaani, kutoziendeleza, kukabiliana nazo na ukweli na kuchagiza wanaozitekeleza kubadili tabia. Na ni baya kwamba hatuwezi kufanya jambo hili peke yetu, tunategemea msaada wa serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na nyie vyombo vya Habari kwa sababu kukabiliana na sumu ya chuki ni wajibu wa kila mtu.””