Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtu 1 kati ya 3 duniani hana fursa ya kupata maji safi ya kunywa na huduma za kujisafi- UNICEF/ WHO 

Watoto wakiteka maji machafu katika mto karibu na nyumbani jimbo la Ruyigi nchini Burundi. Septemba 14, 2017
© UNICEF/UN0185046/Haro
Watoto wakiteka maji machafu katika mto karibu na nyumbani jimbo la Ruyigi nchini Burundi. Septemba 14, 2017

Mtu 1 kati ya 3 duniani hana fursa ya kupata maji safi ya kunywa na huduma za kujisafi- UNICEF/ WHO 

Afya

Ripoti mpya kuhusu pengo la usawa katika fursa ya kupata maji safi ya kunywa na masuala ya usafi  na kujisafi inaonyesha kwamba zaidi ya nusu ya watu wote duniani hawana fursa ya kupata huduma salama za usafi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO, na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mabilioni ya watu duniani wanaendelea kutaabika kutokana na kukosa huduma bora za maji na masuala ya usafi.

Takribani watu bilioni 2.2 kote duniani, ripoti inasema hawana huduma ya maji salama ya kunywa, bilioni  4.2 wengine hawana huduma salama za usafi na wwatu bilioni 3 wanakosa huduma za msingi za shemu za kunawa mikoni.

Ripoti hiyo ya pamoja ya mpango wa ufuatiliaji wa “hatua kuhusu maji ya kunywa na masuala ya usafi :2000-2017, ikilenga kutokuwepo usawa, imebaini kwamba wakati kuna hatua kubwa zilizopigwa  katika kufikia fursa ya msingi ya maji kwa wote, usafi na huduma za kujisafi , bado kuna pengo kubwa katika ubora wa huduma zinazotolewa katika masuala hayo.

“Fursa isiyo kamilifu haitoshelezi " amesema Kelly Ann Naylor mkurugenzi msaidizi wa UNICEF katika masuala ya maji na usafi (WASH) akiongeza kwamba “endapo maji sio masafi na sio salama kwa kunywa au yako mbali sana na endapo fursa ya huduma ya choo si salama na haipatikani basi hatuwahudumii mamilioni ya watoto duniani.Watoto na familia zao hasa kutoka jamii masikini n aza vijijini ndio walio katika hatari kubwa ya kuacha nyuma."

Wakimbizi wa Nigeria ambao walikimbia machafuko katika maeneo yao, wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya maji katika kambi ya Minawao kaskazini mashariki mwa Cameroon (Februari 2019)
UN Photo/Eskinder Debebe)
Wakimbizi wa Nigeria ambao walikimbia machafuko katika maeneo yao, wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya maji katika kambi ya Minawao kaskazini mashariki mwa Cameroon (Februari 2019)

Bi. Naylor amezitaka serikali “kuwekeza katika jamii zao endapo tunataka kuziba pengo la tofauti za kiuchumi na kijiografia na kufikisha huduma hizo ambazo ni haki muhimu za binadamu.”

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba tangu mwanzo wa karne hii watu bilioni 1.8 wamepata fursa ya huduma za msingi za maji ya kunywa lakini hakuna usawa katika upatikanaji, uwepo na kiwango kinachohitajika cha huduma hizo.

Inakladiriwa kwamba mti 1 kati ya 10 bado hana huduma za msingi ikiwemo watu milioni 144 ambao hunywa maji yasiyo salama. Na takwimu zinadhihirisha kwamba watu 8 kati ya 10 katika maeneo ya vijijini wanakosa huduma hizo muhimu.

Naye mmkurugenzi wa afya ya umma, mazingira na masuala ya afya ya jamii wa WHO , Dkt. Maria Neira amesema “nchi zinapaswa kuongeza juhudi mara mbili katika masualaya usafi la sivyo hatutofikia leo la fursa kwa wote ifikapo mwaka 2030. Endapo nchi zitashindwa kuweka juhudi katikamasuala ya usafi , maji salama na khuduma za kujisafi tutaendelea kuishi na maradhi ambayo kitambo yangekuwa yamesalia katika vitabu vya historia. Wekezeni katika maji, usafi na huduma za kujisafi vinapunguza gharama na ni huduma bora kwa jamii katika njia mbalimbali.”

Wakati vitendo vya watu kujisaidia haja kubwa hadharani vimepunguzwa kwa nusu tangu mwaka 2000 kutoka asilimia 21 hadi asilimia 9, watu milioni 673 bado wanaendelea na vitendohivyo ambavyo huvibebesha serikali mzingo mkubwa.

Ripoti inasema katika nchi 39 nyingi zikiwa ni za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara idadi ya watu wanaojisaidia hadharani imeongezeka.

Takwimu za ripoti

Ripoti hiyo imeainisha takwimu mpya zikionyesha kwamba mwaka 2017 watu bilioni 3 walikosa huduma za msingi kama sabuni na mahali pa kunawa mikono nyumbani , wakiwemo karibu robo tatu yao wanapatikana katika nchi zenye maendeleo duni.

Kila mwaka watoto 297,000 wa chini ya umri wa miaka mitano kufariki diunia kutokana na kuhara kunakochangiwa na ukosefu wa huduma za WASH. 

Uchafu na maji machafu pia vinasaidia kusambaza magonjwa kama kipindupindu , kuhara damu, homa ya ini aina A na homa ya matumbo. 

Bi. Naylor amesisitiza kuwa “kuziba pengo la upatikanaji, ubora na uwepo wa maji, usafi na huduma za kujisafi ni lazima kuwe ni kipaumbele cha kila mikakati, mipango na ufadhili wa serikali. Kutotoa kipaumbele katika mipango ya ufadhili wa huduma za afya kwa wote kunaathiri miongo ya hatua zilizopigwa katika kuvinusuru vizazi vijavyo."