Kuwait yarekodi kiwango cha juu zaidi katika miaka 76 iliyopita- WMO

18 Juni 2019

Shirila la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO limetangaza rasmi viwango vya juu zaidi vya joto vilivyorekodiwa kwenye kituo chake huko Mitribah Kuwait cha nyuzi  joto 54 mnamo tarehe 21 Julai 2016 na huko  Turbat, Pakistan mnamo tarehe 28 Mei mwaka 2017 kuwa ni vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa.

Taarifaya WMO iliyotolewa leo imesema viwango vya joto huko Matribah, Kuwait  sasa vinakubaliwa na WMO kama  vya juu zaidi kuwai kurekodiwa eneo hilo la Asia. Kadhalika viwango hivyo ndivyo vya juu zaidi kutambuliwa kuwaia kurekodiwa katika kipindi cha miaka 76.

“Uchunguzi huu unaonyesha kuwa kuna uwezekano  wa kufanyika utafiti wa kina kuhusu hali za hewa sisizo za kawaida. Uchunguzi wa mara kwa mara kama huu utatupa kujiamini zaidi katika kumbukumbu zetu za hali ya hewa ili kuwezesha kubainisha rekodi zinazovunjwa kote duniani na kwa utafiti unohusu mabadiliko yasiyo ya kawaida ya hali ya hewa,” alisema Randal Corveny mjumbe nayehusika na masuala ya hali ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa yisiyo ya kawaida wa WMO.

Kumbukumbu  za mabadiliko ya hali ya hewa yasiyo ya kawaida ya WMO ni pamoja na viwango vya juu zaIdi au vya chini zaidi vya joto, mvua, mvua yenye mawe nyingi, vipindi vya muda mrefu zaidi vya ukame, upepo mkali na hali ya hewa ya anga za za mbali.

Kulingana na kumbukumbu za hali ya hewa isiyo ya kawaida viwango vya juu zaidi vya joto kuwai kurekodiwa  vilikuwa eneo la Furnace Creek, Death Valley, California vya nyusi joto 56.7 tarehe 10 Julai mwaka 1913.

Kamati ya uchunguzi iliwahusu wataalamu wa hali ya hewa kutoka Italia, Kuwait, Pakistan, Saudi  Arabia, France, Uhispania Morocco, Armenia, Iran, Australia, Marekani na Uingereza. 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter