Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu duniani kuzidi bilioni 9 ifikapo mwaka 2050:UN

Mama na mwana Niger.2018
UNFPA/Ollivier Girard
Mama na mwana Niger.2018

Idadi ya watu duniani kuzidi bilioni 9 ifikapo mwaka 2050:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Idadi ya watu duniani inatarajiwa kufikia bilioni 9.7 ifikapo mwaka 2050 na inaweza kuongezeka kwa kasi zaidi na kufika bilioni 11 mnamo mwaka 2100 kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa inayotathimini ongezeko la idadi ya watu duniani.

Ripoti hiyo ya “Matarajio ya idadi ya watu duniani 2019” iliyotolewa leo na kitengo cha  masuala ya idadi ya watu katika idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataia (DESA) inasema ingawa kiwango cha ukuaji kinatofautiana baina ya kanda na kanda nchi nyingi zinashuhudia kupungua kwa idadi ya watu. Idadi ya watu inatarajiwa kuongezeka watu bilioni mbili katika miaka 30 ijayo kutoka idadi ya sasa ya bilioni 7.7 hadi bilioni 9.7 mwaka 2050 na inaainisha mtazamo, mwenendo na matarajio ya idadi ya watu kwa misingi ya kijiografia.

Tathimini ya ripoti

Ripoti hiyo imehitimisha kwamba idadi ya watu duniani huenda ikafikia kilele mwishoni mwa karne hii ambao itakuwa karibu bilioni 11. Ripoti hiyo pia imethibitisha kwamba ongezeko la idadi ya watu linazeeka kutokana na kuongezeka kwa muda wa watu kuishi na kushindwa kwa viwango vya majaribio ya watu kupata watoto na kwamba idadi ya nchi zinazoshuhudia kupungua kwa idadi ya watu inaongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabadiliko ya kiwango ,mchanganyiko na mgawanyo wa idadi ya watu duniani kuna athari muhimu katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.

Makadirio mapya ya idadi ya watu duniani kwa mujibu Ripoti hiyo yanaonyesha kwamba nchi tisa duniani kwa jumla zitakuwa na zaidi ya nusu ya idadi yote ya watu duniani kati ya sasa na mwaka 2050 na nchi hizo ni India, Nigeria, Pakistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, , Ethiopia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Indonesia, Misri na Marekani.  

Na ifikapo 2027 ripoti inasema, India inatarajiwa kuipita China kwa Idadi ya wat una kuwa ndio taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani  .

Mgawanyo wa idadi ya watu:

Idadi ya watu Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara inatarajiwa kuongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2050, ikiwa ni opngezeko la asilimia 99. Na nchi ambazo zinatarajiwa kuwa na kiwango kidogo cha ongezeko la idadi ya watu kati ya sasa 2019 na 2050 ni Ocenia asilimia 56, Afrika Kaskazini na Asia Magharibi asilimia 46, Australia na New Zealand asilimia 28, Asia ya Kati na kusini asilimia 25, Amerika ya Kusini na Caribbea asilimia 18 Mashariki na kusini mashariki mwa Asia asilimia 3 na Ulaya na Amerika Kaskazini asilimia 2.

Kiwango cha uzazi kimataifa ambachi kimepungua kutoka watoto 3.2 kwa mwanamke mmoja mwaka 1990 hadi watoto 2.5 mwaka 2019 kinatarajiwa kupungua zaidi na kufikia watoto 2.2 mwaka 20150.

Makadirio ya uzazi.

Kwa mwaka 2019 ripoti inasema kiwango cha uzazi kwa wastani kimesalia kuwa juu ya watoto 2.1 kwa mwanamke mmoja katika Maisha yake yote, huku Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa ni Watoto 4.6, Ocenia 3.4, Agfrika Kaskazini na Asia Magharibi 2.9 na Asia ya Kati na Kusini 2.4.

Ripoti imesisitiza kuwa kiwango cha uzazi wa Watoto 2.1 kwa mwanamke mmoja kinapaswa kuendelea ili kuhakikisha kuwepo kwa vizazi vinavyo na kuepuka kushuka kwa kiwango hicho kwa muda mrefu kwa kutokuwewpo na uhamiaji.

Bwana. Liu Zhenmin, msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kiuchumi na kijamii amesema “Ripoti hii inatoa mwelekeo wa wapi hatua zichukuliwe na kutiliwa mkazo. Sehemu nyingi ambako kuna ongrezeko kubwa la idadi ya watu ni katika nchi masikini, ambako ongezeko la idadi ya watu linaongeza changamoto katika juhudu za kutokomeza umasikini , kupatikana kwa usawa , kutokomeza njaa na utapiamlo, na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya  na mifumo ya elimu ili kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma.”

Nini kifanyike

Ili kunufaida na ongezeko hilo la idadi ya watu Bwabna. Zhenmin amesema “serikali zinapaswa kuwekreza katika elimu na afya , hususan kwa vijana na kuweka mazingira mazuri ya ukuaji endelevu wa uchumi.

Ripoti inasema hata hivyo watu katika nchi masikini bado wataishi miaka 7 pungufu ya kiwango cha wastani cha umri wa kuishi duniani ambao uliongezeka kutoka miaka 64.2 mwaka 1990 hadi 72.6 mwaka 2019. Na kinatarajiwa kuongezeka Zaidi hadi miaka 77.1 ifikapo mwaka 2050.

Ingawa kuna hatua kubwa zilizopigwa katika kuziba pengo la tofauti ya umri wa watu kuishi bado kuna mapengo mengi yaliyosalia duniani. Makadirio ya 2019 yanaonyesha kwamba umri wa watu kuishi katika nchi zenye maendeleo duni uko chini miaka 7.4 ya kiwango cha wastan duniani kutokana na kiwango kikubwa cha vifo vya Watoto na kina mamam wakati wa kujifungua , machafuko, vita na athari zinazoendelea za HIV.

Inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2050 mti 1 kati ya 6 kote duniani atakuwa na umri wa Zaidi ya miaka 65 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 ikilinganishwa na mwaka 2019 ambapo ni mtu 1 kati ya 11 ndio mwenye umri huo.

Idadi ya watu watakaokuwa na umri wa miaka 80 au Zaidi inatarajiwa kuongezeka mara tatu  kutoka milioni 143 mwaka 2019 hadi milioni 426 mwaka 2050.