Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi Kubwa ya wakimbizi kutoka Venezuela waingia Peru, UN yaingia kusaidia.

Kila asubuhi majira ya saa kumi na moja alfajiri, mamia ya wasichana na wavulana wanavuka mpaka kutoka Venezuela kuelekea kwenye mabasi ambayo yanawapeleka shuleni Cucuta, Colombia.
UNICEF/Arcos
Kila asubuhi majira ya saa kumi na moja alfajiri, mamia ya wasichana na wavulana wanavuka mpaka kutoka Venezuela kuelekea kwenye mabasi ambayo yanawapeleka shuleni Cucuta, Colombia.

Idadi Kubwa ya wakimbizi kutoka Venezuela waingia Peru, UN yaingia kusaidia.

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wiki hii limetuma watu wake katika mpaka wa Peru na Ecuador ili kuzisaidia mamlaka wakati ambao idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji zaidi ya 15,000 kutoka Venezuela wamemiminika kuingia Peru.

Ijumaa ya juma hili lilomalizika, zaidi ya wavenezuela 8,000 walivuka mpaka katika eneo la Tumbes, ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kurekodiwa kwa siku moja. Kati yao, 4,700 waliomba hifadhi nchini Peru, pia hiyo ikiwa ni idadi kubwa katika siku moja pekee.

Federico Agusti ambaye ni mkuu wa UNHCR nchini Peru amesema, “watu wanawasiri katika hali mbaya na mbaya zaidi ya hatari. Baadhi yao wametembea kwa siku 30 au 40 kupitia katika nchi mbalimbali ktika ukanda huu. Tjnawaona watu wanaoogua kutokana na utapiamlo na upungufu wa maji mwilini na pia watu wenye matatizo ya kiafya. Kuna familia nyingi zenye watoto.”

Jumla ya wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela waliokimbilia Peru imefikia 800,000 kwa mujibu wa UNHCR. Na kwa upande wa maombi ya hifadhi, hadi sasa Peru imepokea maombi 280,000 na waliooomba vibali vya ukazi wa muda wamefikia 390,000.

Mamlaka za Peru, UNHCR na wadau wao, yakiwemo mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali, wako katika mpaka ewakifanya kazi kwa saa 24 kusaidia mapokezi, misaada ya kibinadamu, matibabu, taarifa, misaada ya kisheria kwa wakimbizi na wahamiaji katika pande zote mbili za mpaka.

Kutokana na idadi hiyo kubwa ya wakimbizi na wahamiaji, Umoja wa Mataifa umeiomba jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na kuzidsaidia nchi zinazoewapokea kama vile Colombia, Ecuador na Peru.