Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mambo 8 usiyoyafahamu kuhusu fedha ambayo wahamiaji wanaituma katika nchi zao.

Kiasi kidogo cha dola 200 au 300 ambacho kila mhamiaji anatuma nyumbani, kinatengeneza angalau asilimia 60 ya kipato cha familia.
IFAD/Christine Nesbitt
Kiasi kidogo cha dola 200 au 300 ambacho kila mhamiaji anatuma nyumbani, kinatengeneza angalau asilimia 60 ya kipato cha familia.

Mambo 8 usiyoyafahamu kuhusu fedha ambayo wahamiaji wanaituma katika nchi zao.

Ukuaji wa Kiuchumi

Jumapili hii dunia imeadhimisha kwa mara ya pili siku ya kimataifa ya  fedha inayotumwa na wahamiaji kwa ajili ya familia zao zilizosalia nyumbani.

Siku hii huadhimishwa kila tarehe 16 ya mwezi Juni katika kukumbuka mchango muhimu wa wafanyakazi wahamiaji kwa familia na jamii zao nchini mwao.

Yafuatayo ni mambo 8 ambayo unaweza kuwa huyafahamu kuhusu nguvu ya fedha hizi ndogondogo ambazo hata hivyo xzina mchango mkubwa katika maenmdeleo endelevu duniani kote.

 

  1. Takribani mtu mmoja kati ya watu tisa duniani kote wanasaidia na fedha inayotumwa nyumbani na wafanyakazi wahamiaji.

Kwa sasa, takribani watu bilioni moja duniani au mmoja kati ya watu saba wanahusika na fedha inayotumwa nyumbani, iwe kwa kutuma au kuzipokea. Takribani watu milioni 800 duniani au mmoja kati ya watu tis ani wapokeaji wa mtiririko huu wa fedha inayotumwa na wanafamilia ambao wamehamia katika nchi nyingine ili kufanya kazi.

 

  1. Kiasi cha fedha kinachotumwa nyumbani ni asilimia 15 tu ya mapato ya wahamiaji.

Kwa wastani, wafanyakazi wahamiaji wanatuma kati ya dola 200 na 300 kila mwezi au ndani ya miezi miwili. Kinyume na Imani iliyopo, kiwango hiki ni asilimia 15 tu ya kile wanachokipata, kiasi kinachosalia yaani asilia 85 inabaki katika nchi wanamofanya kazi na kinarejea katika uchumi wa nchi hizo walimovuna fedha.

 

  1. Ni gharama kubwa kutuma fedha nyumbani.

Mitandao ya kutuma fedha nyumbani huwa ni ya gharama kubwa, kwa wastani, duniani kote, gharama ya kutuma fecha hufikia asilimia 7 ya jumla ya fedha iliyotumwa. Ili fedha hiyo iweze kuwa na manufaa ni muhimu angalau gharama ya kuituma iwe chini ya asilimia 3.

 

  1. Fedha inayopokelewa ni ya muhimu kuwasaidia mamilioni kutoka katika umasikini.

Ingawa fedha inayotumwa inawakilisha asilimia 15 ya fedha ambayo wafanyakazi wahamiaji wanaipata, mara nyingi ni kiasi kikubwa cha kipato katika familia wanazotoka kwenye nchi zao na kwa hivyo inawakilisha ukombozi katika mamilioni ya familia.

 “Siyo kuhusu fedha inayotumwa nyumbani, ni kuhusu faida ya fedha hiyo katika maisha ya watu wanaotumiwa.” Anaeleza Gilbert F. Houngbo rais wa Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD.

Inakadiriwa kuwa robo tatu ya fedha inayotumwa nyumbani inasaidia katika masuala kama vile chakula, gharama za matibabu, ada za shule na malipo ya nyumba. Pia katika nyakati za majanga, wafanyakazi wahamiaji hutuma fedha nyumbani ili kusaidia pale panapokuwa pametokea uharibifu wa mazao au dharura za kifamilia.

 

  1. Fedha inayotumwa nyumbani inaweza kusaidia kuyafikia angalau malengo saba kati ya 17 ya SDGs.

Wakati wahamiaji wanapotuma fedha nyumbani, wanachangia katika malengo kadhaa ya maendeleo endelevu yanayokusudiwa kuwa yametimizwa kufikia mewaka 2030, mathalani lengo namba mojam kutokomeza umaskini, lengo namba mbili, kutokomeza njaa, lango namba tatu, afya bora na ustawi, lengo namba 4, elimu bora, lengo namba sita, maji safi na huduma za kujisafi, lengo namba nane, kazi bora na ukuaji wa uchumi, lengo namba kumi, kupunguza pengo la kukosekana kwa usawa.

 

  1. Nusu ya fedha inayotumwa nyumbani inaenda moja kwa moja katika maeneo ya vijijini ambako watu mskini duniani wanaishi.

Takribani nusu ya fedha duniani kote inayotumwa nyumbani inaenda katika maeneo ya vijijini ambako robo ya watu maskini duniani wanaishi na ambako hakuna hukakika wa chakula. Inakadiriwa kuwa, dunaini, makusanyo ya fedha kwenda vijijini katika miaka mitano ijayo yatafikia dola trilioni moja.

 

  1. Fedha inayotumwa nyumbani ni muhimu zaidi kuliko misaada ya kimataifa

 

Fedha inayotumwa nyumbani ni chanzo binafsi cha mitaji ambayo ni mra tatu ya kiwango cha misaada rasmi ya maendeleo na uwekezaji wa kigeni kwa pamoja.

Mathalani kwa mwaka 2018, zaidi ya wafanyakazi wahamiaji milioni 200 walituma dola bilioni 689 katika nchi zao ambapo kiasi cha dola bilioni 529 zilienda katika nchi zinazoendelea.

Vilevile kwa mujibu wa IFAD ni kuwa kiasi cha fedha kitakachotumwa na wafanyakazi wa kimataifa kwa familia zao katika nchi zinazoendelea kinategemewa kupanda na kufikia zaidi ya dola bilioni 550 katika mwaka huu wa 2019, ikiwa ni ongezeko la dola bilioni 20 ikilinganishwa na kiwango cha fedha zilizotumwa mwaka 2018.

 

  1. Umoja wa Mataifa unafanya kazi kusaidia utumaji fedha nyumbani, kote duniani.

Bwana Houngbo rais wa IFAD anasema, “ni sawa kabisa kusema kuwa, katika maeneo maskini ya vijijini, fedha inayotumwa inaweza kusaidia kwa vizazi vijavyo kufanya uhamaji kuwa jambo la kuchagua na si la lazima.”

Kwa hivyo kwa mchango huo wa wahamiaji katika maendeleo kupitia fedha inayotumwa nyumbani, ni moja ya malengo ya mkataba wa kidunia uliofikiwa na Umoja wa Mataifa mwezi desemba mwaka jana 2018 kuhakikisha uhamaji salama, uliopangwa na wa kawaida.