Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajasiriamali wakutana Niger kujadili ajira kwa vijana:IOM

Mwanamke akinunua tende kwenye soko moja lililoko mji wa Bol, nje kidogo ya mji mkuu wa Chad, N'djamena.
OCHA/Pierre Peron
Mwanamke akinunua tende kwenye soko moja lililoko mji wa Bol, nje kidogo ya mji mkuu wa Chad, N'djamena.

Wajasiriamali wakutana Niger kujadili ajira kwa vijana:IOM

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Wajasiriamali ambao ni wamiliki wa biashara na miradi mipya 75 wakutana mjini Niamey Niger ili kujadili changamoto kubwa ya upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini humo.

Kila mwaka ukosefu wa fursa za ajira , hali mbaya ya hewa na umasikini uliokithiri huwalazimisha vijana wengi kutoka Niger kufungasha virago na kuikimbia nchi yao kwenda kusaka maisha bora ama kwa muda au moja kwa moja.

Ili kuwasaidia vijana nchini Niger shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM mwezi Januari mwaka jana lilizindua mradi kwa ajili ya maendeleo ya wajasiriliamali (IDEE). Mradi huo lengo lake kubwa ni kusaidia biashara za mashinani kutoa fursa za ajira kwa vijana nchini Niger.

Na jana Alhamisi Juni 13 IOM iliandaa mkutano wa tatu wa kitaifa iliojumuisha wanafaika 75 wa mradi wa IDEE na washiriki zaidi ya 100 walihudhiria mkutano huo wakiwemo wa kitaifa na kimataifa.

Kupitia shughuli zake mradi wa IDEE unasaidia kuhamasisha vijana kuanzisha fursa za kazi mashinani na shughuli za ujasiriliamali kana mbadala wa vijana hao kufungasha safari na kuwa wahamiaji wasio rasmi, lakini pia mradi unazingatia mahitaji ya makundi yaliyo hatarini kama wanawake na watu wenye ulemavu.

Mradi huo pia unachagiza vijana kusoma elimu ya juu, kuanzisha sekta nyingine za kiuchumi kama masuala ya teknolojia IT au mitindo ili kuweza kupata fursa za ajira bunifu kuwasaidia vijana wenzao.

Kwa mujibu wa IOM Zaidi ya asilimia 75 ya Waniger ambao wameajiriwa hivi sasa wanafanya kazi katika sekta ya kilimo ambayo ndio mwajiri mkubwa nchini Niger.

Kwa mwaka jana pekee IDEE imewasaidia wajasiriamali 36 nchini Niger na wengine 39 waliohitimu vyuo vikuu walio na mawazo ya biashara bunifu . 

Wafaidika hao wote wamewasilisha mawazo yao ya biashara jana kwenye mkutano huo na kubadilishana mawazo na vijana wengine huku watatu ambao tayari wako katika mradi walipatiwa tuzo kwa kutambua mchango, mafanikio na ajira walizoweza kuwapa vijana wenzao.

Mradi wa IDEE unafadhiliwa na wizara ya mambo ya nje ya Italia na shirika la Italia la ushirikiano na maendeleo (AICS) na kutekelezwa na IOM ikishirikiana na wizara ya vijana na ujasiriliamali ya Niger, Caital Finance na shirika lisilo la kiserikali la Terre Solidali.

 

TAGS: IOM, Niger, vijana, IDEE, AICS, Italia, ajira