ILO hakikisheni uwepo wa mazingira salama na yenye afya kazini:UN

13 Juni 2019

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu hii leo wamelitaka Shirika la Kazi Duniani ILO mara moja kutambua na kuanza kutekeleza suala la mazingira salama na yenye afya kazini kama moja ya haki za kimsingi kazini.

“Mamilioni ya watu kote duniani wanasumbuliwa na magonjwa na ulemavu kutokana na mazingira yasiyo salama ya kufanyia kazi. Inakadiriwa kuwa takriban wafanyakazi milioni mbuli hufa mapema kila mwaka kutokana kafanya kazi katika mazingira yasiyo salama,” wamesema wataalamu hao wakati wa mkutano wa ILO ulioandaliwa mjini Geneva Uswis.

Mazingira salama na yenye afya ya kazi yanatambuliwa chini ya Makubaliano ya Kimataifa ya Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni tangu mwaka 1966 kama haki ya kimsingi ya uwepo mazingira bora ya kufanyia kazi.

Wataalamu hao huru walisema nchi na biashara mara kwa mara wameeleza kufuata maelekezo ya Umoja wa Mataifa yanayohusu biashara na haki za binadamu yanayoshirikisha wajibu wa kuhakikisha wafanyakazi wana mazingira salama na yenye afya. wataalam hao wameongeza kuwa 

Hata hivyo ni jambo la kujutia kuwa baadhi ya waajiri na mashirika yanayowawakilisha wanajaribu kuzuia kutambuliwa kwa haki ya mazingira salama na yenye afya kama moja ya haki ya kimsingi ya ILO, hali ambayo imeibua maswali kuhusu kujitolea kwa sekta ya kibinfasi katika kuheshimu haki za binadamu.

Hatua ya ILO ina umuhimu wa kuhakisha ukomo wa kunyanyaswa wafanyakazi ambao wanalazimika kuchagua kati ya mshahara na afya zao. Ni jamboa la kuhusunisha kwa mamilioni ya watu ambao wamepoteza maisha yao kutokana na chaguo hilo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud