Mradi wa UN umenikomboa mimi na familia yangu DRC:Feza Hamis

13 Juni 2019

Umoja wa Mataifa umeendelea na kampeni ya kukomesha ukatili na unyanyasai wa kingono katika maeneo yenye mizozo huku ukiimarisha miradi ya kuwasaidia waathirika wa janga hilo. Nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo , DRC  Umoja wa Mataifa umewasaidia  wanawake wengi waathirika kwa miradi mbalimbali. John Kibego na tarifa zaidi

DRC ambayo bado inaghubikwa na vita kwa miongo kadhaa sasa maelfu ya watu wamefungasha virago kwenda kusaka usalama lakini waliosalia wengine wanakabiliwa na changamoto ya Ebola hivi sasa huku wanawake wengi wakikumbwa na ukatili na unyanyasaji wa kingono na kijinsia. Kwa walionusurika na unyanyasaji wa kingono maisha ni magumu na hata kujikimu wao na familia zao inakuwa mtihani mkubwa.

Lakini sasa kupitia mafunzo ya ujasirimali yanayoendeshwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO na ofisi maalumu ya miradi ya kuwasaidia waathirika wa unyanyasaji na ukatili wa kingono (SEA) kwenye operesheni za ulinzi wa amani, yamewapa matumaini ya maisha wanawake hao na miongoni mwao ni Feza Seluwa Hamisi

SAUTI YA FEZA HAMISI

Na tangu alipopata mafunzo haya hadi sasa Feza anasema mradi huo umekuwa mkombozi kwake na familia yake

SAUTI YA FEZA HAMISI

MONUSCO na ofisi hiyo ya msaada kwa waathirika wa SEA wanasema kipaumbele chao kwa wanawake hawa ni kuhakikisha wanajitegemea na kumudu familia zao .kwa kujiajiri wenyewe kupitia ujuzi wanaoupata ikiwemo wa kuoka mikate, ushonaji, na kilimo.

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter