Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto aliyeugua Ebola Uganda afariki dunia

Safari za mpakani kutoka Sudan Kusini hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC zinazua hofu ya uwezekano wa Ebola kusambaa.
UN Photo/Beatrice Mategwa
Safari za mpakani kutoka Sudan Kusini hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC zinazua hofu ya uwezekano wa Ebola kusambaa.

Mtoto aliyeugua Ebola Uganda afariki dunia

Afya

Wizara ya afya nchini Uganda leo limesema kwamba mgonjwa aliyethibitishwa wiki hii kuwa na Ebola nchini humo amefariki dunia. 

Taarifa iliyotolewa leo na wizara ya afya ya Uganda imesema mgomnwa huyo ambaye alikuwa ni mtoto mwenye umri wa miaka mitano kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo DRC amefariki dunia kwenye kituo cha afya cha Ebola cha Bwera alikokuwa akipatiwa matubabu baada ya kuwasili na familia yake kutoka nchini DRC. Pia wizara hiyo imesema ndugu wawili wa familia yake wamepimwa na kuthibitika kuwa na virusi vya Ebola pia. 

Kisa hiki kimethibitishwa katika wilaya ya Kasese amabyo inapakana na jimbo la Kivu ya Kaskazini ambako usalama usio thabiti umekuwa ukikitatiza juhudiza kudhibiti virusi vya ebola.

Dkt. Jane Ruth Aceng, Waziri wa Afya wa Uganda amesema, baada ya vipimo vya sampuli ya damu kutoa matokeo chanya ya virusi vya ebola, mgonjwa huyo ambatye ni mtoto mwenye umri wa miaka 5, amelanzwa kwenye chumba maalum kilichowekwa tayari kushughulikia wathirika wa ebola kwenye hospitali ya Bwera.

Ameongeza kuwa, mtoto Allan Bwambale amerejea hivi karibuni kutoka vijiji vya Masambu kule Beni nchini Jmahuri ya Kidemokrasaia ya Congo (DRC), alikokwenda na mamaye kuhudhuria mazishi ya babu yake aliyeshuliwa kufariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya ebola.

Ebola Uganda?

Bwambale ni mtu wa kwanza kabisa kuambukizwa Ebola nchini Uganda tangu mlipuko wa ebola utangazwe nchini DRC, mwezi Mei mwaka jana.

Kisa cha Bwambale kimeripotiwa wakati ambapo wizara ya afya na wadau wake likiwemo shirika la afya ulimwenguni (WHO), wameimarisha juhudi za kuzuia ebola kuenea hadi huku Uganda. 

Uganda ilimalizia kutangaza mlipuko wa eola mwaka 2012 ambao ulisababisha vifo vya watu 17 wilayani Kibaale.

Kifo hicho kimetokea wakati huu ambapo shirika la afya Ulimwenguni (WHO), limethibitisha vifo 1,208 kufuatia mlipuko wa ebola uliotangazwa nchini Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), tarehe 8 mwezi Mei, mwaka 2018, Wizara ya Afya katika nchi jirani ya Uganda imethibitisha kisa cha kwanza cha ebola nchini humo katika wilaya ya moja ya mpakani. 

Kinachozidisha uwezekano wa virusi hivyo kuenea maeneo mengine ya Uganda hasa yale yanayopakana na majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini ni mizozo ya bunduki inayolazimisha maelfu kusaka hifadhi Uganda, na pia maingiliano ya kibiashara na kijamii kwani watu wengi wa mpakani wana jamaa zao katika nchi jirani.Hivyo Waziri Aceng amehimiza wanchi wote kuwa chonjo Zaidi na kuripoti kisa chochote kinachoshukiwa kuwa ni ebola haraka iwezekanavyo.