Tukishikamana na kuchukua hatua tunaweza kuzuia migogoro kupitia usuluhishi:Guterres

12 Juni 2019

Tukishikamana na kuchukua hatua mapema tunaweza kufanikiwa kuzia migogoro isiendelee na hivyo kuokoa Maisha ya mamilioni ya watu na kuwapunguzia madhila na kutekeleza moja ya jukumu kubwa zaidi la Umoja wa Mataifa lilioainishwa kwenye katiba.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu kuzuia migogoro na upatanishi.

Guterres amesema “kuzuia migogoro na upatanishi ni nyenzo mbili muhimu sana tulizonazo zinazoeweza kuwapunguzia binadamu machungu wanayopitia wakati wa machafuko na vita, tunashirikiana na pande husika katika migogoro na wadau wengine katika kanda nan chi kote duniani ili kutimiza malengo haya.”

Hata hivyo Katibu Mkuu amesema kuna dalili za matumaini ikiwemo mafanilio yaliyopatikana nchini Mali na Madagascar kwa kuzingatia katiba katika ubadilishanaji wa madaraka.

Amesema mfano mwingine ni muafaka baina ya Eritrea na Ethiopia wa hivi karibuni na hata kukufuka kwa matumaini ya amani Sudan kusini. Pamoja na matumaini haya Guteres amesema “kwingineko tunakabiliwa na changamoto kubwa za juhudi zetu, lakini tunaendelea kusonga mbele na safari hii.”

Kinachohitajika kufanyika

Katbu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterre, akihutubia Baraza la Usalama leo 12 Juni 2019 lilipokutana kujadili suala la uzuiaji wa migogoro na usuluhishi
UN /Loey Felipe
Katbu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterre, akihutubia Baraza la Usalama leo 12 Juni 2019 lilipokutana kujadili suala la uzuiaji wa migogoro na usuluhishi

Katibu mkuu amesema mathalani makubaliano yaliyofikiwa Stockholm na pande husika katika mzozo nchini Yemen ilikuwa hatua muhimu na sasa inapaswa kusonga mbele katika majadiliano ya muafaka na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo anafanyakazi kwa karibu na pande zote ili kusaidia uetekelezaji wa makubaliano ya Hudaidah ili kuzuia kurejea kwa vita.

Kwa upande wa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR Guterres amesema Umoja wa Mataifa unasaidia pande husika katika utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Muungano wa Afrika AU, kuendesha operesheni za kuhakikisha makundi yaenye silaha yanazingatia makubaliano na kuwezesha mikataba ya amani ya kimaeneo.

Na kwa upande wa Burkina Faso amesema Umoja wa mataifa unashirikiana na wadau  mbalimbali wa kitaifa ikiwemo asasi za kiraia na makundi ya wanawake kuimarisha miundominu kwa ajili ya amani kama sehemu hatua za kukabiliana na machafuko ya kidini.

Mustakabali wa amani bado uko njiapanda

Bwana. Guterres amesema licha ya juhudi zote hizi amani bado inakabiliwa na vikwazo vingi.”Mgawanyiko katika jumuiya ya kimataifa unamaanisha kwamba vita vinaendelea kusambaa huku washiriki wa nchi wakivitazama au kuvichochea zaidi na raia ndio wanaolipa gharama kubwa.”

Taarifa yake pia imesema kuna ongezeko la ubinafsi na será zoinazochangia chuki, kutenga walio wachache na idtikadi Kali na hata katika jamii ambazo haziko katika vita.

Amesisitiza kuwa kuna majaribio katika baadhi ya nchi “kurudisha nyuma masuala ya haki za binadamu na hata mchakato ambao umekuwa ukifanyika katika miongo ya karibuni kuhusu masuala ya jinsia na ujumuishwaji, huku nafasi ya asasi za kiraia ikiendelea kupungua.”

Katika maeneo mengine kama Libya Guterres ameelezea jinsi machafuko yanayoendelea yanavyoendelea kuwabebesha mzingi mkubwa raia hususan wanawake na watoto na pia kukosekana kwa ari ya kumaliza vita hivyo.

Wakimbizi kutoka Venezuela wanaolekea nchi jirani mjini  Cúcuta,Colombia wakielekea Pamplona.
© UNHCR/Stephen Ferry
Wakimbizi kutoka Venezuela wanaolekea nchi jirani mjini Cúcuta,Colombia wakielekea Pamplona.

Kuhusu Venezuela amesema hali ya kibinadamu ni mbaya sana na inatia hofu kubwa  na kwamba kwas asa Umoja wa Mataifa unaunga mkono juhudi za kimataifa zinazoendelea kusaka siuluhu ya amani ambazo zinafanyika nchini Norway.

Akiangazia Syria,  Katibu mkuu amesema bado kuna changamoto kubwa na taifa hilolinakabiliwa na hali ya mzunguko wa machafuko , kutokuwepo na utulivu na madhila makubwa kwa raia.Amesisitiza kuwa “hatuwezi kuwa na amani endelevu wakati makundi tofauti yanaendeleza operesheni za kijeshi nchini humo.Hakuna suluhu ya kijeshi katika mzozo huu, bila suluhu ya kisiasa ambayo itazingatia azimio la baraza la usalama namba 2254 Syria asilani haitokuwa na utulivu au amani.”

Katiba ya Umoja wa Mataifa

Guterres amekumbusha kwamba kipengele cha 1V cha katiba ya Umoja wa Mataifa kimeainisha nyenzo kadhaa kwa ajili ya pande kinzani kuzitumia kuzuia na kutatua migogoro. Nyezo hizo ni pamoja na “majadiliano, uchumuzi, upatanishi, maridhiano, kukiri, muafaka wa kisheria, kutumia mashirika ya kikanda au mipango, au njia zingine za amani za chaguo lao.”

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu amezitaka serikali kutumia nyenzo hizo na pia amelitaka BNaraza la Usalama kutumia mamlaka yake kutoa wito kwa pande husika katika mizozo kuzingatia nyenzo hizo. Ameongeza kuwa maendeleo endelevu pia ni njia mojawapo ya kuzuia migogoro na amesema ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anashikiriki na kushirikishwa. 
amesisitiza kuwa washiriki binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo wazee ni muhimu sana katika kufanikisha juhudi hizo.

Amelitaka pia Baraza na nchi wanachama kuhakikisha mshikamano ili kuhakikisha uzuiaji na upatanishi vinawezekana, akisema hiyo ndio njia pekee ya kutimiza wajibu wetu kwa watu tunaowahudumia.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter