Bachelet akaribisha uamuzi wa mahakama kuu Botswana kuhalalisha LGBT

11 Juni 2019

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet leo amekaribisha uamuzi wa mahakama kuu ya Botswana wa kuhalalisha uhusiano wa hiyari wa wapenzi wa jinsia moja miongoni mwa watu wazima kwa kuondoa baadhi ya vipengele vya sharia za nchi hiyo.

Kwa kauli moja mahakama kuu imebaini kwamba sehemu ya sheria iliyokuwa ikiharamisha uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja kuwa ni kinyume na katiba na unakiuka haki za binadamu ikiwemo uhuru wa fargha, usawa, uhuru na utu.

Bi Bachelet amesema “huu ni uamuzi wa kihistoria ambao utawaweka huru wasagaji, mashooga, wanaofanya mapenzi ya jinsia zote na waliobadili jinsia (LGBT) nchini Botswana dhidi ya aina mbalimbali za ubaguzi na vikwazo vilivyotokana na vipengelele hivyo vya sheria .”

 

OHCHR/Joseph Smida
LGBTI wakiwa katika maandamano

Ameongeza kuwa “kuwaadhibu watu kutokana na mwelekeo wao wa kimapenzi kunaathiri mbaya sana ambazo zinaenda mbali zaidi ya hatari ya kukamatwa na kswekwa jela.Kuharamisha LGBT kunachangia unyanyapaa na kuruhusu kusambaa kwa ubaguzi na kusambabisha watu hao kunyimwa huduma za afya, elimu, ajira na nyumba.”

Bachelet amepongeza umuhimu wa jukumu la mahakama nchini humo kwa kuhakikisha iko huru na isiyoegemea upande wowote katika kushughulikia masuala yanayokiuka haki. “Naipongeza Botswana kwa uamuazi huu wa kihistoria na kupongeza mashirika ya LGBT nchini Botswana pamoja na washirika wao kwa ujasiri na maono ya kupigania haki kwa watu wote wa taifa hilo."

Botswana ni nchi ya 9 katika kipindi cha miaka mitano kuhalalisha uhusiano wa hiyari wa wapenzi wa jinsia moja. Uamuzi kama huo umepitishwa pia na mahakama au wanasheria katika nchi za Angola, Belize, India, Msumbiji, Nauru, Palau, Ushelisheli, na Trinidad na Tobago.

 

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter