Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 95 wauawa nchini Mali, MINUSMA yalaani vikali

Katika picha hii ya maktaba, wanakijiji kutoka  Ogossagou,  jimbo la  Mopti  nchini Mali baada ya shambulio la tarehe 23 Machi mwaka 2019 na kusababisha vifo vya watu 160 na wengine 70 walijeruhiwa, mamia kupoteza makazi.
UNICEF/Maiga
Katika picha hii ya maktaba, wanakijiji kutoka Ogossagou, jimbo la Mopti nchini Mali baada ya shambulio la tarehe 23 Machi mwaka 2019 na kusababisha vifo vya watu 160 na wengine 70 walijeruhiwa, mamia kupoteza makazi.

Watu 95 wauawa nchini Mali, MINUSMA yalaani vikali

Amani na Usalama

Mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia Mali ni ukatili usiostahili na unaopaswa kushughulikiwa haraka, umesema leo mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA baada ya shambulio la jana jioni kukatili maisha ya raia wengi kwenye Kijiji cha Sobanou-Kou kilichopo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Bandiagara, kwenye jimbo la Mopti.

Kwa mujibu wa taarifa za awali watu wenye silaha walivamia Kijiji hicho na kufanya mashambulizi yaliyokatili maisha ya takriban watu 95 na kujeruhi wengine wengi, na idadi hii imethibitishwa na vyanzoi rasmi na walioshuhudia kilichoendelea.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Mali Bw. Mahamat Saleh Annadif amesema “nimeshitushwa na kughadhibishwa na shambulio hili katikati mwa Mali, nalaani vikali kitendo hili ya kikatili pamoja na machafuko,. Ninatoa wito kwa mamlaka nchini Mali kufanya uchunguzi haraka dhidi ya janga hili na kuwafikisha wahusika kwenye mkono wa sheria.”

Ameongeza kuwa "na kwa bahati mbaya zahma hii inatukumbusha kwamba machafuko yanayoendelea hakuna watu wabaya upande mmoja na wazuri upande wengine, kila mmoja anahusika na kiwango cha uvumilivu kimefikia ukomo na ni lazima wakati huu serikali kushika hatamu . MINUSMA itawajibika kikamilifu."

Bwana Annanadif ametuma salamu za rambirambi kwa waathirika wa shambulio hilo , watu na serikali ya Mali. 

Ameongeza kuwa tangu asubuhi ya leo MINUSMA imekuwa ikiratibu msaada kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Mali na kwamba mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Mali unahamasisha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa watu walioathirika na zahma hiyo.

MINUSMA kwa sasa imepeleka operesheni za ulinzi katikati mwa Mali kwa lengo la kuisaidia vikosi vya ulinzi na usalama vya Mali katika juhudi zao za kuwalinda raia.