Uchafuzi wa hali ya hewa warejesha hadhi ya baiskeli China:UNEP

4 Juni 2019

Kwa muda sasa magari yamechukua nafasi ya usafiri wa baiskeli katika miji mingi ya China , lakini kutokana na ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa ambalo ni tatizo kubwa katika taifa hilo la Asia sasa baiskeli zimeanza kurejea kwa kishindo, kwa msaada mkubwa wa teknolojia na ubunifu wa karne ya 21.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP kuna wakati China hata ilikuwa ikichukuliwa kama ufalme wa baiskeli , ambapo baiskeli zilitawala mitaa karibu yote ya miji ya taifa hilo , lakini katika miongo minne iliyopita ukuwaji mkubwa wa kiuchumi nchini humo ukichanganywa na ukuaji wa miji vimeshuhudia watu wengu wakizipa kisogo baiskeli na kuingia katika magari kama ndio njia yao kuu ya usafiri na kuchakia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa hewa.

 

Vijana wakiendesha baiskeli kandoni mwa jengo ambalo ni urithi wa UNESCO magharibi mwa  mji mwa Hangzhou. China
Yimin Feng
Vijana wakiendesha baiskeli kandoni mwa jengo ambalo ni urithi wa UNESCO magharibi mwa mji mwa Hangzhou. China

Hangzhou mji ambako maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mazingira duniani hapo kesho Juni 5 yatafanyika kuna wakati ulielezwa kuwa ni mji bora zaidi duniani, lakini sasa uchafuzi wa hali ya hewa umesababisha athari kubwa, na takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO zinaonyesha kuwa uchafuzi huo mjini Hangzhou umepita kiwango salama cha WHO.

Hata hivyo katika jitihada za kuboresha afya ya umma na mazingira malaka ya mji wa Hangzhou imeweka msisitizo katika kuendesha baiskeli ambazo zimeundwa kidijitali na kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na hali ya hewa, na miji mingine imeanza kufuata nyayo.

Katika muongo mmoja uliopita serikali ya mji huo imekuwa ikiboresha miundombinu na kuifanya iwe rafiki zaidi kwa watumiaji wa baiskeli ikiwemo kuweka ishara za barabari na njia maalum kwa ajili ya waendesha baiskeli pia serikali ya mji huo imegawa takriban baiskeli 86,000 kwa umma.

Pia kuemanzishwa kadi maalum ya kusafiria ambao humfanya msafiri kuwa na fursa ya kutumia vyombo vyote vya usafiri kuanzia baiskeli, boti hadi mabasi.” Kwa ujumla kumekuwa na safari milioni 760 za baiskeli , hiyo ni karibu nusu ya watu wote nchini China” amesema Tao Xuejunmeneja mkuu wa mradi wa huhuma za umma za baisklei mjini Hangzhou na kuongeza kwamba “Hadi sasa miji zaidi ya 400 nchini China imefuata nyayo za mradi wetu, ndoto zetu ni kuchagiza mtindo huu kwa China nchima na duniani kote”.

Maegesho ya baiskeli kandoni mwa jengo ya urithi wa dunia la UNESCO katika mji wa Hangzhou, China
Yimin Feng
Maegesho ya baiskeli kandoni mwa jengo ya urithi wa dunia la UNESCO katika mji wa Hangzhou, China

 

 

Matokeo ya mradi huu kwa mujibu wa Tao usafifiri wa baiskeli umekuwa chaguo kubwa na maarufu kwa wenyeji na watalii na juhudi za kampuni inayoendesha zoezi hilo ambayo inaendeshwa na serikali imetunikiwa tuzo ikiwemo kutambulika kimataifa na kupatiwa tuzo ya kimataifa ya Ashden kwa kuwa na usafiri endelevu mwaka 2017.

Apu ya simu za rununu ambayo inapanda mamilioni ya miti

Mbali ya kuongoza katika kufufua matumizi ya baiskeli China mji wa Hangzhou pia ni maskani ya kuchagiza Maisha endelevu ya kisasa, na ukiwa na apu ambayo inasaidia kukomesha ukataji miti, kupunguza uchafuzi wa hewa na kupanda mamilioni ya miti mipya.

Programu ya apu hiyo iitwayo “Ant Forest” ambao ni mradi mhsusi kwa ajili ya mji wa Hangzhou kutoka kwa kampuni ya malipo na muundo wa Maisha ya china kuputia apu ya Alipay inawachagiza na kuwashawishi watu kuchukua hatua ndogo za kulinda amazingira kila siku kama vile kuendesha baiskeli badala ya kuendesha magari kwenda kazini au kurejelea nguo hizohizo badala ya kununua mpya kila wakati anasema Annie Hao mhasibu wa kampuni ya fedha ya Ant ambayo ndio muasiusi wa Alipay.“ Kila wakati ninapochukua hatua ya kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa ninatunzwa kwa kupewa pointi za nishati inayolinda mazingira na nikishakusanya pointi za kutosha mti halisi unapandwa na hadi sasa miti Zaidi ya milioni 13 imeshapandwa heko kwa hatua za watumiaji milioni 300 wa apu hiyo.

(PHOTO)

Kwenye miji kama Beijing nchini China, ukungu ni tatizo kubwa la kiafya.
WMO/Alfred Lee
Kwenye miji kama Beijing nchini China, ukungu ni tatizo kubwa la kiafya.

 

Vita vya Beijing dhidi ya uchafuzi wa hewa

Kimataifa moja ya mifano halisi ya athari za uchafuzi wa hali ya hewa jinsi unavyoathiri kiwango cha Maisha katika mji ni mji mkuu wa China Beijing. Maendeleo makubwa mjini Beijing katika miongo miwili iliyopita yameshuhudia ongezeko kubwa la uchafuzi wa hewa kutokana na sababu mchanganyiko ikiwemo uchafuzi utokanao na makaa yam awe, kukuwa kwa sekta ya magari hususani malori makubwa ya kusafirishia mizigo, viwanda vikubwavikubwa na vumbi kutoka katika ujenzi wa nyumba na barabara.

Hii ni kutokana na mmoja wa waandishi wa ripoti ya umoja wa Mataifa isemayo:”Tathimini ya miaka 20 ya udhibiti wa uchafuzi wa hali ya hewa Beijing.”

Chembechembe zinazotokana na uchafuzi huoi wa hewa China zinasababisha vifo na magonjwa. Leo hii uchafuzi wa hewa mjini Beijing ni mara 7.3 ya kiwango salama cha hewa cha kila mwaka kilichowekwa na WHO lakini serikali za miji na kikanda nchini humo zimejitahidi kukabiliana na hali hiyo na kuboresha kiwango cha hewa katika miaka ya karibuni.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNEP kanda ya Asia Pasifiki Dechen Tsering “Beijing imefikia kiwango kinachotia matuiani cha hewa safi katika muda mfupi , ni mfano mzuri wa jinsi gani mji mkubwa katika nchi ziinayoendelea unavyoweza kuweka uwiano wa ulinzi wa mazingira na ukuaji wa uchumi.

China ndio mwenyeji wa maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya mazingira duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Juni 5 , na mwaka huu ikibeba kaulimbiu “uchaguzi wa hewa” maadhimisho yatakayofanyika mjini Hangzhou.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter