Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mr. Eazi na Sherrie Silver na kampeni ya kuinua vijana vijijini

Sherrie Silver akitoa mafunzo kwa wakulima vijana kijijini Cameroon kwa ajili ya video ya muziki kuchagiza wakulima vijana.
©IFAD/DavidPacqui
Sherrie Silver akitoa mafunzo kwa wakulima vijana kijijini Cameroon kwa ajili ya video ya muziki kuchagiza wakulima vijana.

Mr. Eazi na Sherrie Silver na kampeni ya kuinua vijana vijijini

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umezindua mpango bunifu wa kufungua fursa za kilimo kwa vijana vijijini hususan kwenye maeneo ambayo ni masikini zaidi ili hatimaye kutokomeza njaa na umaskini.

Ni kibao hiki Freedom chake  mwanamuziki mashuhuri barani Afrika Oluwatosin Ajibade maarufu kama Mr. Eazi[IZI] alichorekodi upya mahsusi kwa ajili ya mpango huo wa kufungua fursa za vijana waishio vijijini.

Kibao hiki ambacho wamerekodia nchini Cameroon wakiwa na vijana wa vijijini, kinasema kuwa ushiriki wa kilimo, ni uhuru zaidi kwa mtu.

Mr. Eazi anaungana na mshindi wa tuzo ya MTV na muandaa miondoko ya dansi Sherrie Silver ambaye pia ni mchechemuzi wa IFAD kwa ajili ya vijana vijijini kutaka vijana wajirekodi kupitia apu ya TikTok kwa sekunde 15 wakicheza kibao hiki kwa miondoko ya Sherrie.

Jina la kampeni ni #DanceforChange yaani dansi ili ulete mabadiliko kwa lengo la kutokokomeza njaa na umaskini ambapo Sherrie anasema,

(Sauti ya Sherrie Silver)

“Vijana waishio vijijini barani Afrika na kwingineko duniani wanakimbia vijijini kutokana na ukosefu wa rasilimali, ukosefu wa ajira na msaada. Tunaamini kwenye uwezo wa vijana kulisha dunia yenye njaa. TikTok ni apu kubwa ya kuandaa video kwa hiyo na ushirikiano na IFAD tunaamini tunaweza kuleta mabadiliko makubwa.”

IFAD itatumia dansi zilizorekodiwa na vijana ikiwa na #DANCEFORCHANGE kuwasilisha rasmi ombi kwa viongozi kuongeza ufadhili kwenye kilimo na kufungua fursa zaidi kwa vijana vijijini.

Kwa mujibu wa IFAD hivi sasa duniani kote kuna vijana bilioni 1.2 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo zaidi ya asilimia 80 ya idadi hiyo wanaishi nchi zinazoendelea na walio vijijini bado uwezo wao haujatumiwa vya kutosha.