Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 Tunalaani vikali mauaji ya mfanyakazi wa UN Galkayo:UNSOM

Kikosi cha ulinzi cha Umoja wa Mataifa (UNGU) kikiwa kazini katika mnara mjini Moghadishu Somalia
UN /Ilyas Ahmed
Kikosi cha ulinzi cha Umoja wa Mataifa (UNGU) kikiwa kazini katika mnara mjini Moghadishu Somalia

 Tunalaani vikali mauaji ya mfanyakazi wa UN Galkayo:UNSOM

Amani na Usalama

Kaimu mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM na naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Somalia Raisedom Zenanga amelaani vikali mauaji ya mfanyakazi msaidizi wa idara ya ulinzi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia Mohamed Abdi Khayre

Kwa mujibu wa Zenanga Khayre ambaye ni mfanyakazi wa kitaifa raia wa Somalia alipigwa risasi na watu wasiojulikana jana jioni alipokuwa akitoka msikitini mjini Galkayo. Alikimbizwa hospitali lakini baadaye alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata, na hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote lililodai kuhusika na mauaji hayo ya Bwana. Khayre.

Bwana Zenanga amesema “Tunaomboleza kifo cha Khayre ambaye alifanya kazi kwa ufanisi mkubwa na utendaji mahiri kwenye idara ya ulinsi ya Umoja wa Mataifa wakati wa uhai wake kwenye shirika hili. Tunaitaka serikali kufanya kila juhudi kumsaka mtu aliyempiga risasi na kufanya mauaji haya ya kikatili ya mfanyakazi mwenetu aliyekuwa na ujasiri mkubwa ambaye aliweka maisha yake rehani kwa ajili ya kuwalinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walioko mjini Galkayo.Familia nzima ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia inatuma salamu za rambirambi kwa falimia, ndugu na marafiki wa bwana Khayre.”