Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hongera Antigua na Barbuda kwa kupiga marufuku matumizi ya mara moja ya plastiki:PGA

Raiswa Baraza Kuu Maria Fernanda Espinosa
UN Photo/Mark Garten)
Raiswa Baraza Kuu Maria Fernanda Espinosa

Hongera Antigua na Barbuda kwa kupiga marufuku matumizi ya mara moja ya plastiki:PGA

Tabianchi na mazingira

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo amekaribisha azimio jipya lililopitishwa nchini Antigua na Barbuda la kuchukua hatua dhidi ya matumizi ya mara moja plastiki ambazo huchafua mazingira.

Azimio hili litatiwa saini katika tamasha maalum lililopewa jina ‘Play it out” nlitakalofanyika kesho Juni Mosi nchini Antigua kama sehemu ya kampeni ya kimataifa inayoendeshwa na Rais huyo wa Baraza Kuu Maria Fernanda Espinosa dhidi ya uchafuzi wa mazingira unakanao na plastiki na matumizi ya mara moja ya plastiki .

Azimio hilo la Antigua na Barbuda ni hatua muhimu sana yenye lengo la kuzichagiza nchi zote za visiwa vya Carribea kuchukua hatua zaidi za kutokomeza kabisa matumizi ya mara moja ya bidhaa za plastiki  na kusitisha uchafuzi wa mazingira ya bahari.

Bi. Espinosa ambaye anawasili Antigua na Barbuda leo kwa ajili ya tamasha hilo la Jumamosi anaamini kwamba azimio hilo sio tú la kihistoria bali pia ni la muhimu na linaweza kutekelezeka. 

Kwani amesema linadhihirisha uongozi madhubuti katika kuchukua hatua dhidi ya plastiki na haja ya haraka n aimara ya kukabiliana na tatizo la plastiki.

 Antigua na Barbura na mataifa ya kwamnza katika nchi za kundi la Amerika ya Kusini na carribea (GRULAC) kuchukua hatua hiyo muhimu dhidi ya matumizi ya mara moja ya plastiki.

Tamasha hilo la “Play it out” litakalofanyika Jumamosi litajumuisha watu mashuhuri akiwemo mshindi wa tuzo za muziki za Grammy Ashanti, mfalme wa soka wa Machel Montano kutoka Trinidad and Tobago, na wasanii wengine wa kimataifa kama Bomba Estereo, Nico na Vinz, Robin Schulz, Rocky Dawuni, na St. Lucia.