Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nguvu ya vijana wa bara la Afrika, zinaendeleza bara hilo kuelekea enzi mpya za maendeleo endelevu-Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihudhuria mkutano wa sayansi,teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) kuhusu programu za kompyuta.
UN Photo/Antonio Fiorente
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihudhuria mkutano wa sayansi,teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) kuhusu programu za kompyuta.

Nguvu ya vijana wa bara la Afrika, zinaendeleza bara hilo kuelekea enzi mpya za maendeleo endelevu-Antonio Guterres.

Masuala ya UM

Nguvu na matumaini ya vijana isiyo na mipaka ya vijana wa kiafirika vinaimarisha bara hilo kuelekea katika nyakati mpya za maendeleo endelevu, sambamba na ushirikiano mpya kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU. Hiyo ni kwa mujibu wa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alioutoa hii leo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Afrika.

Mapema mwaka huu, Bwana Guterres alikuwa katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambako alitumia muda kukaa na wasichana wanafunzi kutoka katika mataifa 34 ya Afrika ambao wanajifunza masuala ya program za komputa.

“Hawakuwa wanaendeleza tu ujuzi wao; walikuwa wanatoa changamoto na kwa ubaguzi wa kijinsia na wanahamasisha ushirikishwaji katika teknolijia ya kidijitali ambayo itakuwa muhimu katika kulipeleka bara la Afrika katika mstakabali stahimilivu na wenye hewa kidogo ya ukaa.”Amesema Bwana Guterres.

Siku ya Afrika inaadhimisha kutimia kwa miaka 56 ya kuanzishwa kwa Umoja wa nchi huru za kiafrika ambao hivi sasa ni Muungano wa Afrika yaani AU.

Bwana Guterres pia anasema, “tangu nilipotwaa madaraka mwaka 2017, nimeweka kipaumbele kwenye ushirikiano wa kimakakati kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika. Ninajivunia kusema kumekuwa na wingi wa ushirikiano wetu kuanzia katika kuimarisha kitaasoisi mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika hadi kwenyempango kazi mpya kati ya pande hizi mbili katika masuala ya amani, usalama na maendeleo endelevu, pamoja na maazimio ya pamoja ya ushirikiano katika operesheni za amani.Tunasaidia jitihada za AU katika kuzuia machafuko na pia katika maafikiano ikiwemo kunyamazisha bunduki ifikapo mwaka 2020.”

Kwa kutumia malengo ya pamoja ya kutokomeza umaskini, Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa na AU wanafanya kazi pamoja katika kuimarisha Agenda ya mwaka 2030 na Agenda yam waka 2063 katika mipango ya maendeleo na kushirikiana katika kufungua fursa mpya kutoka katika eneo huru la biashara la Afrika.

Amehitimisha kwa kusema ushirikiano wa kimkakati kati ya Umoja wa Mataifa na AU tayari umeanza kuleta matokeo na kwahivyo,”hebu tujenge katika misingi hii imara ili kufanya ushirikiano wetu uwe na ufanisi zaidi, kupitia kuheshimiana na kutegemeana.”