Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bachelet asikitishwa na hatua ya mahakama kuu Kenya kazia vizuizi vya uhalifu mahusiano ya jinsia moja

Bendera za jamii ya LGBTI
UNAIDS (file)
Bendera za jamii ya LGBTI

Bachelet asikitishwa na hatua ya mahakama kuu Kenya kazia vizuizi vya uhalifu mahusiano ya jinsia moja

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet leo ameelezea kusikitishwa na uamuzi wa mahakama kuu ya Kenya ya kukazia hukumu ya sheria ya zama za ukoloni ya kutohalalisha mahusiano ya jinsia moja kati ya watu wazima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Mahakama Kuu ya Kenya ilikuwa imeombwa kuangalia upya kipengele cha 162 na 165 cha sheria ambavyo vinatoa fursa ya vizuizi vya kisheria kuweza kutumika kwa watu ambao wanahukumiwa na vitendo vya ngono vya watu wa jinsia moja.

Watetezi wa haki za binadamu kwa muda mrefu wamesema kwamba mapendekezo haya yanakiuka wajibu wa haki za binadamu wa Kenya na vinachangia katika ukatili na unyanyapaa dhidi ya watu wa makundi ya wasagaji, mashoga, wenye uhusiano wa pande mbili na waliobadili jinsia zao, LGBT.

Bi. Bachelet amenukuliwa katika taarifa akisema, “kufanya kuwa uhalifu vitendo ambavyo vinalenga kundi moja kwa misingi ya wanaowapenda na walivyo ni unyanyapaa. Aidha inatoa ujumbe hatari kwa jamii kwa ujumla na inaibua uhasama n ahata ukatili dhidi ya LGBT.”

Halikadhalika ameongeza kwamba, “kunyimwa haki ya elimu, afya na makazi na ajira vyote vinaweza kuelekezwa kwa kutajwa kama uhalifu mahusiano ya kinsia moja.”

Kamishna Mkuu amesema kwamba harakati za LGBT na wadau wake Kenya wamepigana kuhakikisha haki za jamii ya LGBT. 

Ameongeza kwamba, “ujumbe wangu kwa watu wa Kenya ni kuendelea kupigana kwa ajili ya usawa kwa wote na kutokataa tamaa. Umoja wa Mataifa unasimama pamoja na ninyi na unaungana na nyinyi katika azma yenu ya hadhi, haki sawa na usawa."

Maamuzi ya Mahakama Kuu ya Kenya ni tofauti na maamuzi ya hivi karibuni na watunga sharia katika nchi zingine kote ulimwenguni ambazo zilizofutilia sheria za kufanya kuwa uhalifu mahusiano ya watu wa jinsia moja. 

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Angola Belize, India, Msumbiji, Nauru, Palau na Ushelisheli na Trinidad na Tobago zimefutilia kuwa uhalifu tendo la mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja.