Mafundi seremala Kigoma wapatiwa mbinu za kutengeneza mizinga bora ya nyuki

24 Mei 2019

Nchini Tanzania mashirika ya Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa pamoja wa Kigoma, KJP yamekuwa yakitekeleza miradi mbalimbali ili kusaidia kusongesha maendeleo ya mkoa huo ambao kwa miaka kadhaa umekuwa ukipokea wakimbizi kutoka nchi jirani.

Miongoni mwa miradi ya hivi karibuni zaidi ni ule wa kuwezesha wafugaji wa nyuki katika wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma kutumia mbinu bora za ufugaji nyuki ili kusaidia kuongeza kipato na kulinda mazingira.

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO nchini Tanzania hivi karibuni liliendesha mafunzo si tu kwa wafugaji wa nyuki bali pia mafundi seremala ili hatimaye waweze kutengeneza mizinga bora ya nyuki kwa kutumia miti iliyopandwa badala ya ile ya asili ili kutunza mazingira sambamba na kusaidia wafugaji kupata mizinga ya kisasa kama anavyoelezea fundi seremala huyu.

Sauti ya Fundi Seremala

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud