Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fistula yaendelea kuwa jinamizi kwa wanawake wakati wa kujifungua:UNFPA

Daktari akizungumza na mmoja wa wagonjwa wa Fistula.
UNFPA/Ollivier Girard
Daktari akizungumza na mmoja wa wagonjwa wa Fistula.

Fistula yaendelea kuwa jinamizi kwa wanawake wakati wa kujifungua:UNFPA

Afya

Licha ya tahadhari na jitihada kubwa zinazofanyika kote duniani kuwanusuru, ugonjwa wa Fistula umeendelea kuwa ni jinamizi linalowaghubika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA. 

Fistula ni ugonjwa ambao husababisha shimo kubwa kati ya njia ya uzazi na njia ya mkojo unatokana na mama kuwa na uchungu wa muda mrefu bila matibabu. Kwa mujibu wa UNFPA mara nyingi ugonjwa huu huwapata wanawake na wasichana masikini kabisa na wanaotoka jamii zilizotengwa.

Katika ujumbe kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambayo kila mwaka huadhimishwa Mei 23, mkurugenzi mtendaji wa UNFPA Dkt. Natalia Kanem katika ujumbe wake amesema “wasichana na wanawake walioathirika na ugonjwa huu ambao unazuilika na kwa kiasi kikubwa kutibika mara nyingi wanakosa huduma na matokeo yake, wanakabiliwa na unyanyapaa mkubwa katika kijamii. Kukosa kwao uwezo wa kupata matibabu ya haraka sio tu kunawapokonya afya zao na utu wao bali pia ni ukiukwaji wa haki zao za binadamu”

Ameongeza kuwa wakati mwingine wasichana na wanawake hawa hufuata masharti yote wakati wa ujauzito na bado bahati mbaya huwakuta wakati wa kujifungua mfano Keflene Yakobo kutoka Tanzania aliyeolewa na mri wa miaka 17 na kupata ujauzito akiwa na umri wa miaka 19. Akizungumza na UNFPA amesema alizingatoia masharti na maagizo yote.” Nilianza kuhudhuria kliniki punde tu nilipotambua niña ujauzito na hadi miezi yote tisa lakini wakati wa kujifungua mambo yalibadilika na kuwa mabaya na nilipata Fistula moja ya majeraha mabya kazisa yanayotokea wakati wa kujifungua.”

Na kama walivyo wanawake wengi wanaokabiliwa na Fistula mume wa Bi Yakobo alimuacha muda mfupi tu baada ya kurejea nyumbani toka hospital na kubaini ana Fistula” Umekuwa ni wakati mgumu sana katika maisha yangu , watu walinicheka, zikuweza hata kuhudhuria shughuli zozote za kijamii, sikuweza hata kwenda kanisani wala kuwatembelea marafiki zangu, wanajamii wengine walinitenga kwa sababu ya hali yangu.”

Kituo cha afya cha huduma ya kijamii kisicho cha serikali kijulikanacho kama  CCBRT ambacho kilimsaidia Bi Yakobo kwa kumfanyia upasuaji maalum, kinasema kila mwaka wanawake 3000 nchini Tanzania hupata Fistula.

Nazo takwimu za UNFPA zinakadiria kwamba takriban wanawake takriban milioni 2 Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, Asia, ulimwengu wa Kiarabu, Amerika Kusini na Caribbea wanaishi na Fistula na visa vipya kati ya 50,000 hadi 100,000 hutokea kila mwaka duniani kote.

Shirika la afya duniani WHO linatesema tatizo hilo la Fistula linaweza kuepekwa kwa wasichana kuchelewa kupata mimba ya kwanza, kwa kuachana na mila potofu kama ukeketaji, na kupata huduma za afya ya uzazi mapema.