Ghassan Salama: Watu milioni 6.5 Libya wanaohistahili amani

Tripoli, Libya picha ya maktaba ikionesha wananchi wakikusanya mizigo yao kwa ajili ya kuhama baada ya kupata vitisho kutoka kwa wapiganaji.
UNHCR/Tarik Argaz
Tripoli, Libya picha ya maktaba ikionesha wananchi wakikusanya mizigo yao kwa ajili ya kuhama baada ya kupata vitisho kutoka kwa wapiganaji.

Ghassan Salama: Watu milioni 6.5 Libya wanaohistahili amani

Amani na Usalama

Mamilioni ya watu nchini Libya wameteseka vya kutosha na sasa wanastahili amani kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa leo kwenye Baraza la Usala na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Libya.

Mwakilishi huyo Ghassan Salameh amesema "Ripoti hii, ambayo nimekuwa nikifanya kazi kwa miaka miwili iliyopita, haiepukiki."

Miongoni mwa yaliyoainishwa katika ripoti yake ni siku arobaini na mbili za mashambulizi yaliyoanzishwa na vikosi Field Marshal Hfter mjini Tripoli ambayo yameacha mamia wakipoteza Maisha na na uharibifu, na sasa Libya imeghubikwa na machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaweza kusababisha mgawanyiko wa kudumu nchi humo , akiongeza kwambaurejeshaji katika hali ya kawaida zahma inayoendelea sasa Libya itachukua miaka mingi.

Miaka 8 tangu kuondolewa kwa utawala wa Ghadaffi nchini Libya, bado nji ya kuelekea katika amani na usalama imesalia kizungumkuti.
OCHA/Giles Clarke
Miaka 8 tangu kuondolewa kwa utawala wa Ghadaffi nchini Libya, bado nji ya kuelekea katika amani na usalama imesalia kizungumkuti.

Hali halisi ya machafuko

Kwa mujibu wa mwakilishi huyo, machafuko hayo mjini Tripoli yamekatili Maisha ya watu zaidi ya 460, na 29 kati yao ni raia, huku wengine Zaidi ya 2,400 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa ni raia.

Pia ripoti imesema  raia zaidi ya 75,000 wamelazimika kukimbia makwao, hasa wanawake na watoto. Watu wengine 100,000, wakijumuisha wanawake na watoto bado wamekwama katika maeneo ya mapigano.

Salameh  pia ameelezea wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka kwa kasi kwa vitendo vya uporaji, unyang’anyi,  kutoweka na watu kuswekwa kizuizini kiholela tangu mwanzo wa mgogoro wa sasa. Maafisa angalau saba wa usalama pia wamekuwa wakiwekwa kizuizini au kufungwa katika maeneo ya  Mashariki na Magharibi mwa Libya. Wakati hatma ya watu hawa bado haijulikani, Salameh amesisitiza umuhimu wa kujali utu wa wat una usalama wao.

Mwakilishi huyo Maalum ametaja pia kuendelea kumomonyoka kwa masuala ya kijamii nchini Libya kutokana na machafuko yanayoendelea, akielezea kuwa "sauti ya vyama vya ndani ya nchi na kikanda kwa vzimefunika sauti za wito wa ukomeshaji uhasama na maridhiano baina ya pande zinazopigana ambazo zinatumia mifumo ya uendeshaji wa vyombo vya habari kama silaha kwa kusambaza habari za uongo na uvumi zinazochochea chuki."

Na amesisitiza kwamba mgogoro wa Libya hauwezi kutatuliwa kijeshi, Ghassan Salameh ni kwa njia ya mchakato wa kisiasa tu na haiwezekani kupuuza vita inayoendelea kama kwamba haipo na haikutokea. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa, kama mpatanishi asiye na upendeleo, ni lazima iendelee na kasi ya mchakato huo ili  kuzipa  pengo kubwa la kutoaminiana linaloghubika mvutano huo tangu ulipoanza .

Watu walioshikiliwa kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli, wakisubiri kuhamishiwa eneo salama. Pichani Msichana kutoka Eritrea mwenye umri wa miaka 19 akizungumza na mfanyakazi wa UNOCHA akisubiri kupanda basi kuelekea kituo cha mpito kabla ya kwenda Niger.
UN OCHA/GILES CLARKE
Watu walioshikiliwa kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli, wakisubiri kuhamishiwa eneo salama. Pichani Msichana kutoka Eritrea mwenye umri wa miaka 19 akizungumza na mfanyakazi wa UNOCHA akisubiri kupanda basi kuelekea kituo cha mpito kabla ya kwenda Niger.

Matumaini ya mustakbali bora

Ghassan Salameh amesema mafanikio ya maisha bora ya baadaye kwa ajili ya taifa la Libya bado inawezekana, lakini kuna haja ya haraka ya kuchukua hatua sasa kabla ya vita kushika kasi zaidi katika vitongoji wenye watu watu wengi kwenye  mji mkuu. Na hili ameongeza linahitaji mshikamano na uratibu wa haraka wa jumuiya ya kimataifa "Kama watendaji na watu wenye ufahamu wa ngazi za kimataifa na kikanda tunatambua kwamba Libya si tunu tu ya kupokelewa kwa mikono miwili bali , ni nchi inayokaliwa na watu milioni 6.5 wanaostahili amani na haki ya kuchagua mustakabali wao kwa pamoja. Hofu yangu hapo baadaye ni kwamba Libya itakuwa hatarini na naogopa athari za kushindwa kuchukua hatua haraka ili kujagiza kurejea katika mchakato wa mazungumzo ukishirikisha pande zote kwani hivi sasa Libya inatumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na hali itakayochangia mganwanyiko mkubwa wa taifa hilo. "

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akikutana na wakimbizi na wahamaiaji katika kituo mjini Tripoli, Libya. 4 April 2019.
UN Spokesperson/Florencia Soto Niño
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akikutana na wakimbizi na wahamaiaji katika kituo mjini Tripoli, Libya. 4 April 2019.

 Nini kifanyike

Salame amesema “Wito wangu kwa Walibya ni kuacha mapigano sasa kwa ajili ya wapendwa wao na nchi yao na kwa ajili ya amani na usalama wa kimataifa, na ninaliomba Baraza la Usalama kutimiza  wajibu wake wa kuhimiza ukomeshaji wa uhasama . Na wito kwa pande zote kinzani nawaomba mshirikiane na kufanya kazi na ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha nia ya ukomeshaji mapigano na kurejea kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya mchakato wa kisiasa unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Pia amevitaka vyombo vya Habari nchini Libya kutokuwa silaha ya kusambaza chuki , kupitia Habari za uongo, za bandia na uzushi. Amesema ili kufanikisha azma yam ani lazima pengo la kutoaminiana lizibwe na linahitaji kuzibwa sasa kabla ya kuleta zahma kubwa Zaidi nchini Libya.