Madhila tunayopitia kama wakimbizi toka Cameroon hayasemeki: Agah

17 Mei 2019

Machafuko yanayoendelea katika majimbo ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Cameroon yamewalazimu maelfu ya watu kufungasha virago na kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi, huku wengi wakivuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Nigeria bila chochote.

Kwenye makazi ya wakimbizi ya Okende nchini Nigeria Rachal Agah miongoni mwa wengi kutoka Cameroon anasema yeye ni mjane, mumewe alipigwa risasi na kumuacha na Watoto wane. Maisha ni magumu kama wakimbizi wengine takribani 7000 wanaoishi kwenye kambi hiyo yenye uwezo wa kuhifadhi watu 4000 ahaha kukabiliana na maisha. Rachel anasema

RACHEL AGAH 

“Si rahisi kuondoka nchini kwako na kwenda kutaabika katika nchi nyingine

Yeye na wakimbizi wengine sasa wanategemea msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR

RACHEL AGAH

“Kila siku na kila usiku nawaza, ninawaza kuhusu mgogoro nchini Cameroon na kuhusu marehemu mume wangu”

Josiah Flomo ni mkuu wa ofisi ya UNHCR Ogoja

SAUTI YA JOSIAH FLOMO

Hatuna rasilimali za kutosha katika masuala yote tunayoyapa kipaumbele, suala la usajili, la chakula, la maji, malazi, afya, na elimu kwa sababu hatuna ufadhili wa kutosha kuweza kutoa msaada unaohitajika kukidhi mahitaji yao”

UNHCR iliomba dola milioni 184 kusaidia wakimbizi wa Cameroon na inahofu kwamba idadi ya wakimbizi hao itaongezeka na madhila yataendelea. Rachel ana ujumbe maalum

SAUTI YA RACHEL AGAH

“Huu ni ujumbe ninaowapa huku machozi yakinibubujika, fikisheni ujumbe wangu kwa watu kwamba tunateseka, mateso ni makubwa sana hatutaki kuona halii hii tena.”

 Raia wa Cameroon wanaozungumza lugha ya Kiingereza walianza kukimbia machafuko Oktoba mwaka 2017 na wengi kumiminika Nigeria, na hadi sasa walioorodheshwa kama wakimbizi Nigeria ni 30,000 huku wanawake na watoto wakiwa ni asilimia 80

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud