Kama hakuna fursa ya kufanya utakacho, jitengenezee fursa hiyo:mkimbizi Sadaf 

16 Mei 2019

Sadaf msichana aliyezaliwa na kukulia Afghanistan akighubikwa na vikwazo vingi ikiwemo dini na hata utamaduni, haikuwa rahisi kwake  na hasa akihofia kutotimiza ndoto yake ya kusoma hadi chuo kikuu na kupata ajira.

Katika chumba cha mazoezi nchini Hispania ambako sasa ni mkimbizi ikiwa ni mbali na nyumbani atokako Afghanstan ambako Sadaf anasema siku moja alikuwa anaangalia filamu ambayo ilibadili Maisha yake.

Filamu hiyo ilimuhusu aliyekuwa mfalme wa masumbwi duniani Mohamed ali na sehemu ya filamu hiyo ilimuonyesha Mohamed Ali akifanya mazoezi na binti yake Laila.Na ndipo sadaf akaamua naye pia anataka kuwa mwanamasumbwi,na baada ya miaka michache sadaf akawa miongoni mwa timu ya kwanza ya ndondi ya wanawake Afghanistan, alishiriki mashindano mengi na kujishindia medali.

(SAUTI YA SADAF )

“Nataka kuonyesha jinsi gani binti mdogo kutoka Afghanistan ambaye hawezi hata kutoka nje anapambana na kupigana masumbiwi kwa ajili ya amaisha yake, hili ndio lengo langu. Kama hakuna fursa ya kufanya unachotaka unaitengeneza fursa hiyo mwenyewe.”

Mtengenezaji wa filamu wa Hispania Juan Antonio Moreno Amador aliamua kutengeneza filamu kuhusu changamoto za Sadaf na alifunga safari hadi Afghanistan

(SAUTI YA JUAN MORENO AMADOR)

“Ukumbi wa Filamu ilitualika sote kuvunja miiko yetu na kubadilika kama binadamu. Na hadithi kama hii ya msichana mdogo mwanamasumbwi akipigania uhuru wake, akipigania utu wake pia, siku zote inakuwa mfano kwetu sote .”

Umaarufu wa Sadaf ulipoongezeka yeyé na familia yake walianza kupata vitisho na akihofia maisha yake na kutokuwa tayari kuacha ndondi, Sadaf alijua salama pekee ni kuondoka Afghanistan. Na 2017 alipoalikwa kwenye uzinduzi wa filamu “kupigana kwa ajili ya uhuru” nchini Hispania, Sadaf alitumia fursa hiyo kuomba hifadhi ya kuishi nchini humo ambayo hatimaye alipewa. Hivi sasa amejifunza lugha ya Kihispania na anafanyakazi kwenye mradi wa manispaa ya mji wa Madrid, pia  anatumai siku moja kurejea ulingoni na kuwa mfano wa kuwachagiza na kuwahamasisha wasicha wenzie aliowaacha Afghanistan kupigania ndoto zao

(SAUTI YA SADAF )

“Kuna mambo mengi ambayo wanawake nchini Afghanistan wanataka kufanya lakini hawawezi kusema. Nataka wapate haki zao na kufuata nyayo zao.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter