Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa dharura unahitajika kuzuia vifo Somalia wakati watu milioni 2 wakikabiliwa na njaa-FAO

Maeneo yaliyoathiriwa na  ukame nchini Somalia, angalia mabwaya yaliyotengenezwa kwa kuzingirwa na mchanga yanakuwa suluhu ya muda mfupi kwa wakazi wa eneo hili la Puntland
UNDP Somalia/Said Isse
Maeneo yaliyoathiriwa na ukame nchini Somalia, angalia mabwaya yaliyotengenezwa kwa kuzingirwa na mchanga yanakuwa suluhu ya muda mfupi kwa wakazi wa eneo hili la Puntland

Msaada wa dharura unahitajika kuzuia vifo Somalia wakati watu milioni 2 wakikabiliwa na njaa-FAO

Tabianchi na mazingira

Ukame mkubwa unaoshuhudiwa nchini Somalia huenda ukasababisha njaa kwa watu milioni 2.2 ikiwa ni takriban asilimia 18 ya watu nchini humo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba limeonya leo shirika la chakula na kilimo duniani, FAO.

FAO imetoa angalizo mahsusi kuhusu Somalia ikisema kwamba idadi ya watu walio na njaa inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 40 zaidi ya makadirio ya mapema mwaka huu wa 2019.

FAO imeongeza kuwa mvua za miezi Aprili na Mei zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika uhakika wa chakula kwa mwaka mzima kwani zinategemewa kwa mavuno ya mwaka ya mwezi Julai.

Ukosefu wa mvua katika baadhi ya maeneo kwa mfano eneo la Shabelle ambako kunazalishwa asilimia 60 ya mahindi umeshudiwa na katika eneo la Bay kunakopandwa mtama.

Ukame unaathiri wafugaji na mifugo yao

Mvua chache zimeathiri wafugaji na mifugo yao kwani maeneo ya malisho yanakauka na maji hayapatikani, aidha FAO imeonya kuhusu idadi kubwa ya mifugo yenye afya mabaya kwa sababu ya uzito mdogo na magonjwa yatokanayo na ukame katika maeneo ya katikati na kaskazini mwa nchi.

FAO imeongeza kwamba baadhi ya wakulima wamelazimika kuchinja baadhi ya mifugo yao kutokana na ukosefu wa maji na lishe kwa mifugo na kujaribu kuokoa mifugo inayokamuliwa.

Huko Puntland, Somalia, mimea inakauka, mifugo inakufa kutokana na ukame kwenye eneo hilo, kufuatia mfululizo wa miaka mitatu ya ukosefu wa mvua (Picha ya mwaka 2017).
UNDP Somalia/Said Isse
Huko Puntland, Somalia, mimea inakauka, mifugo inakufa kutokana na ukame kwenye eneo hilo, kufuatia mfululizo wa miaka mitatu ya ukosefu wa mvua (Picha ya mwaka 2017).

Hatua zinahitajika kuzuia vifo

Ukame na kumalizika haraka akiba ya chakula, ikijumuishwa na kudorora kwa ajira na mishahara duni, upunugfu wa bidhaa zitokanazo na mifugo, mizozo nakupungua kwa misaada ya kibinadamua tangu mapema mwaka 2019 kumechangia katika kudidimia kwa uhakika wa chakula nchini Somalia.

FAO inaimarisha juhudi zake ili kudhibiti kudorora kwa hali ya kibinadamu kutokuwa mbaya zaidi. Kwa mantiki hiyo FAO inahitaji fedha zaidi ili kufikia watu milioni 2 walioathirika na ukame mw ahuu kwa kuwapatia msaada wa dharura muhimu kama vile pesa taslimu, mbegu zinazostahimili ukame, vifaa na huduma zingine za kilimo kwa ajili ya upanzi wkati wa msimu ujao.

Aidha FAO imesema ili kulinda mifugo waliosalia, wafugaji wanahitaji msaada wa maji na malisho. Hali kadhalika kampeni za afya ya mifugo zinahitaji kufanyika haraka iwezekanavyo ikianza na matibabu ya dharura kwa mifugo ili kuhakikisha uzima wao.

Kufikia sasa FAO ina pengo la dola milioni 115 la ufadhili nchini Somalia.