Siku ya familia itumike pia kupaza sauti za masuala muhimu katika jamii Tanzania

15 Mei 2019

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya familia leo Mei 15, Umoja wa Mataifa unasema licha ya kwamba muundo wa familia unabadilika kote ulimwenguni kufuatia mienendo ya kimataifa na mabadiliko ya demografia lakini bado Umoja huo unatambua familia kama kundi msingi katika jamii. 

Umoja wa Mataifa umetenga siku hii kwa ajili ya kutoa fursa ya kuchagiza uelewa wa masuala yanayoathiri familia ikiwemo kijamii kiuchumi na kidemografia.

Nchini Tanzania, Abdul Dach ambaye ni mmoja wa baba wa familia anasema siku hii ni muhimu na kwamba kuna mambo ya kuzingatia ndani ya familia ikiwemo

(Sauti ya Abdul)

"Ni muhimu kuheshimu haki za watoto lakini pia kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake, kuanzia wazazi hadi watoto."

Siku ya leo inatoa fursa pia ya kujadili haki za kila mwanafamilia bila kujali hali yake ikiwemo watoto wenye  ulemavu wa ngozi ambapo mmoja wa watoto hao Shega Mboya mkazi wa mkoa wa Morogoro nchini Tanzania anasema,

(sauti ya Shega)

"Siku hii inaweza pia kuwa fursa nzuri ya kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu kundi la watu wenye ulemavu wa ngozi kwani iwapo kundi hili linakubalika katika jamii basi wana uwezo wa kuchangia na kusongesha mbele jamii."

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud