Kamishna Mkuu Bachelet ataka uchunugzi kuhusu kifo cha Hassan Toufic Dika wa Lebanon

14 Mei 2019

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ametaka kufanyike uchunguzi wa kina na ulio huru, kuhusu kifo cha mfungwa mwenye miaka 44 - mwanamume raia wa Lebanon Hassan Toufic Dika, kilichotokea tarehe 11 mwezi huu.

Kifo cha Bwana  Dika kilitokea licha ya mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa kuingilia kati ikiwemo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, na mamlaka za Lebanon baada kuibuka madai kuwa aliteswa akiwa gerezani, kufuatia kukamatwa kwake Novemba 2018 ambapo alinyimwa fursa ya kupata matibabu.

Kifo cha Hassan Dika kinaashiria kile kinaonekana kuwa kufeli kwa mfumo ya sheria za nchini Lebanon, alisema Bachelet. Sheria za nchi hiyo zinaonekana kupuuzwa kwa kushndwa kuchunguza madai ya mateso yaliyokuwa na ushahidi kutokana na ripoti za uchunguzi wa kimatibabu na pia kukataa kutoa matibabu.

Bachelet aliendelea kuongeza kuwa sheria zilioonekana kukiukwa tangia wati Bw Dika alikamatwa na vikosi vya usalama vya Lebanon hadi wakati wa kifo chake siku ya Jumamosi. Kwa sababu hizo zote ni lazima ufanyike uchunguzi ulio huru katika pande zote za kesi hii ili kubaini makosa yalikuwa wapi na kuhamisa kuwa hali kama hizo hazitokei tena nchini Lebanon.

Bachelete alisema mateso na dhuluma za aiana yoyote dhidi ya binadamu haviruhusiwi kwa njia yoyote ile chini ya sheria za kimataifa na za nchini Lebanon. Aliendela kusema kuwa ikiwa Bwana Dinka ni kweli aliteswa jinsi ripoti za matibabu zilisema, basi wale waliamrisha na kutekeleza uhalifu ni lazima wawajibishwe sawa na Yule aliyemyima haki yake ya kupata matibabu na yeyote aliyemnyima haki yake hali ya sheria.

Bwana Dika alifariki tarehe 11 Mei mwaka huu wa 2019.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter