Mradi wa IFAD na EU waimarisha uzalishaji na uwezo wa kununua miongoni mwa wakulima Kenya

14 Mei 2019

Nchini Kenya mradi wa pamoja wa serikali kwa ubia na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD na Muungano wa Ulaya,, EU wa kuwapatia wakulima wadogo mtaji umesaidia kuongeza tija na kubadilisha maisha yao.

Takriban wakulima wadogo wadogo milioni 7.5 nchini Kenya ambao wanazalisha asilimia 75 ya mazao ya kilimo hadi hivi karibuni walikuwa wanakosa mtaji wa kununua pembejeo zinazostahili.

Kama hiyo haitoshi, pia walikosa taarifa kuhusu mifumo ya kilimo bora na uhifadhi, hata hivyo mtaji kutoka IFAD, EU na serikali ulilenga kubadili mwelekeo ukianza na wakulima 25,000.

Mradi huo uliozinduliwa miaka miwili iliyopita umeleta mabadiliko kwa wakulima hao akiwemo Sharon Kirui mkulima wa mahindi kutoka magharibi mwa Kenya ambaye kabla ya mradi mazao yake hayakutosheleza mahitaji ya familia licha ya kwamba kilimo ndio tegemeo lake

(Sauti ya Sharon)

Lakini sasa kuna matokeo chanya..

(Sauti ya Sharon)

Kwa upande wake meneja wa programu wa IFAD ukanda huo, Moses Abukari amesema mradi huo umetoa fursa ya kubadilishana mawazo na kuelezea changamoto na kwamba

(Sauti ya Abukari)

“Kupitia programu hii wakulima wanagundua kwamba kuna fursa nyingi kwa sababu tunachukua mfumo wa mnyororo wa thamani, kwani ndio mwelekeo katika siku zijazo.”  

Mnyororo wa thamani ni mpango ambao unazingatia kuongeza thamani  ya bidhaa kuanzia uzalishaji hadi inapomfikia mlaji.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud